UGUMBA KWA MWANAMKE* SABABU,DALILI NA TIBA ZAKE - KABATA

This is the special room for news where you need to settle with!


Breaking

Friday, 15 November 2019

UGUMBA KWA MWANAMKE* SABABU,DALILI NA TIBA ZAKE

-Tulisema ugumba ni kile kitendo au ni ile hali ya mwanamme na mwanamke kujamiiana kwa kipindi cha mwaka mmoja bila kinga yoyte na bado mwanamke hakuweza kupata ujauzito.-Tukasema hali hii inachangiwa na jinsia zote na si mwanamke peke yake kama ilivyozooleka kuamini.-Theluthi moja ya nyumba zenye tatizo hili huwa imeathirika kutokana na mapungufu ya mwanamme,theluthi nyingine kutokana na mwanamke na inayobakia inaathiriwa na matatizo au ya wote wawili au yale ambayo hayaeleweki.-linapotokea tatizo hili, wote wawili wanatakiwa wapimwe ili kujua ni nani kati yao ndiye chanzo cha tatizo.*Tuangalie dosari kwanza za mwanzo za ugumba kwa Mwanamke*
>>Ili mwanamke apate mimba,sehemu zote za mwili wake zinazohusika na uzazi zinatakiwa zifanye kazi inavyotakiwa.*_Hatua katika utengenezaji wa mimba ni kama zifuatazo:_*1.-Moja kati ya ovari mbili za mwanamke lazima iyachie yai lililokomaa2.-Yai hili lazima lisafirishwe na mrija wa uzazi _(fallopian tube)_3.-Mbegu za mwanamme lazima zisafiri hadi kwenye _cervix_, kupitia tumbo la uzazi _(uterus)_ hadi kwenye mrija wa uzazi, kulifikia yai na kulipevusha.4.-Yai lililopevushwa lazima lisafiri kupitia mrija wa uzazi hadi kwenye tumbo la uzazi _uterus_5.-Yai hilo lazima linate kwenye ukuta wa uterus na kuanza kukua} Ugumba kwa mwanamke unaweza kutokana na dosari katika hatua yoyote katika hizo tulizozitaja na mara nyingine kutokana na dosari katika hatua zaidi ya moja.ii} Pamoja na kuwa kuna sababu nyingi za mwanamke kutopata mimba, lakini sababu kuu tatu ndizo zinazohusika zaidi,*Sababu hizo ni;*1.Kushindwa Kuzalisha Mayai _(Anovulation)_-Hili ndilo tatizo ambalo linachangia ugumba kwa wanawake kwa 30% lakini kwa bahati nzuri 70% ya wanawake wenye tatizo hili hupata tiba na kufanikiwa kupata watoto.-Mwanamke mwenye tatizo hili hutoa mayai mara chache au hatoi mayai kabisa.-Chanzo cha tatizo hili huwa ni moja ya yafuatayo:1._Matatizo Ya Homoni_-Matatizo ya homoni ndiyo yenye mchango mkubwa zaidi kwenye kumfanya mwanamke ashindwe kuzalisha mayai.-Uzalishwaji wa mayai hutegemea mchanganyiko wa homoni utakaofanya kazi kwa kuhusiana bila kuvurugwa katika utendaji wake wa kazi.-Kuna matatizo ya aina kuu tatu yanayoweza kuvuruga mpangilio huu.i} Kuzalisha Mayai Yasiyokomaa:ii}Matatizo Ya *Hypothalamus;**Hypothalamus* ni sehemu ya ubongo inayohusika na kutoa ishara kwa tezi ya pituitary _(pituitary gland)_ ambayo nayo huamsha homoni za ovari zinazoruhusu yai kukomaa.- *Hypothalamus* isipofanya kazi yake, mayai hushindwa kufika ukomavu.-Asilimia 20 ya dosari za ukomavu wa mayai husababishwa na matatizo ya *hypothalamus*.iii} Matatizo Ya *Pituitary Gland:*-Tumeona hapo juu kuwa tezi ya *pituitary* inavyohusika katika kukomaza mayai.-Endapo *pituitary* itatoa homoni kwa kiwango kidogo au kikubwa kupita kiasi, ovari zitashindwa kuzalisha na kutoa mayai ipaswavyo.-Hali hii hutokea pale tezi hii inapoharibiwa kwa ajali,-Kunapotokea uvimbe ndani yake au kunapokosekana ulingano wa kikemikali ndani ya tezi hiyo.
2.*Makovu Kwenye Ovari*i} Uharibifu kwenye ovari unaweza kusababisha ovari hizi kushindwa kuzalisha mayai.ii}Operesheni za mara kwa mara hujenga makovu kwenye ovari hizo na kuzifanya zishindwe kuzalisha mayai.iii} Maambukizi ya magonjwa huweza pia kusababisha ovari kushindwa kuzalisha na kutoa mayai.3.*Kukoma Hedhi Mapema*i} Kukoma hedhi mapema ni tatizo ambalo halijaeleweka vizuri kisayansi.-Baadhi ya wanawake wanaacha kupata siku zao zakawaida kwenye umri usiotegemewa.ii} Dhana moja ni kuwa hifadhi yao ya mayai imekwisha au nyingine ni kuwa inatokana na wanawake hawa kuwa wenye historia ya kuwa wanariadha waliokuwa na miili yenye uzito mdogo na waliofanya mazoeziya nguvu kwa muda mrefu.iii} Kuna uwezekano pia kukoma hedhi mapema ni suala la urithi.4.*Matatizo Ya Follicle*i} Kuna tatizo lisilo na maelezo ya kisayansi “unruptured follicle syndrome” ambapo mwanamke hutengeneza mfuko wa kawaida wa yai wenye yai ndani yake kila mwezi lakini mfuko huo hugoma kupasuka na kuachia yai.} Hivyo kwamba, yai hubaki ndai ya ovari na utolewaji wa yai nje ya ovari kutotokea.5.*Mirija Ya Uzazi*i} Fallopian Tubes_ Kushindwa Kufanya Kazi Vizuri-Magonjwa katika mirija ya uzazi huathiri 25% ya wanafamilia ambapo tatizo laweza kuwa dogo la kunata kwa yai au kubwa la mirija kuzibwa kabisa.ii} Tiba kwa matatizo ya mirija ya uzazi mara nyingi ni upasuaji.>>> _Matatizo yanayopelekea kuziba kwa mirija ya uzazi ni kama yafuatayo:_i} _Maambukizi Ya Wadudu_-Maambukizi ya virusi na bacteria yanayoenezwa kwa ngono husababisha makovu na uharibifu, kwa mfano kama umesha wahi kupima na ukaambiwa una *Hydrosalpnix* hii inasababisha mirija ya uzazi kuziba pande zote na kujaa maji.ii} _Magonjwa ya Tumbo_-Magonjwa ya _*appendicitis na colitis*_ huleta madhara kwenye tumbo ambayo yanaweza kuiathiri mirija ya uzazi kwa kujenga makovu au kuiziba.iii} _Upasuaji_-Hii ni sababu kubwa ya magonjwa na uharibifu wa mirija ya uzazi,kivipi-Upasuaji wa kwenye maeneo ya kinena na tumbo huweza kusababisha uharibifu utakao zuia upitaji wa yai.iv} _Mimba Ndani Ya Mirija Ya Uzazi _(Ectopic Pregnancy)_-Mimba zinazotunga ndani ya mirija ya kizazi huweza kuleta uharibifu kwenye mirija hiyo hata kama tahadhali ya juuitachukuliwa kuziondoa.v} _Matatizo Ya Kuzaliwa Nayo_-Mara chache huweza kutokea kuwa mwanamke akazaliwa akiwa na dosari katika mirija yake ya uzazi.*Endometriosis*Endometriosis* ni kuota kwa seli *(endometrial cells)* zinazofanana na zile zinazotanda ndani na nje ya mfuko wa uzazi _(uterus)_ kwenye eneo nje ya mfuko wa uzazi. *Endometrial cells* ndizo zinazoufunika mfuko wa uzazi na seli hizi hubadilishwa kila mwezi wakati wa hedhi.-Seli hizi huweza kuota kwenye maeneo mengine yaliyo nje kabisa ya mfuko wa uzazi na huitwa *endometriosis implants*.-Maeneo ambayo seli huweza kuota ni kwenye _ovari, mirija ya uzazi (fallopian tubes), kuta za nje za nyumba ya uzazi, utumbo, pelvis, uke, cervix, kibofu na mara chache kwenye maini, mapafu na ubongo_.-Endometriosis imegundulika zaidi kwenye kundi la wanawake wenye umri kati miaka 22 na 35, ingawa mara chacheimeonekana kwa wasichana wadogo wa miaka11.-Endometriosis ni nadra kuonekana kwa wanawake waliokoma hedhi.-Wanawake warefu , wembamba wenye uzito mdogo huonekana zaidi na tatizo hili.-Kupata ujauzito katika umri mkubwa sana, kutozaa na kukoma siku mapema huongeza uwezekano wa kutokea *endometriosis*.-Kuota kwa seli hizi za ziada –na tendo la kuziondoa kwa operesheni –huweza kusababisha makovu ambayo huweza kuzuia yai la mwanamke lisiungane na mbegu ya mwanamme.-Kuathirika kwa utando huu juu ya _uterus_ huweza kuzuia kutungwa kwa yai lililopevushwa._Sababu Nyinginezo_1.*Sababu Za Kitabia*i} Baadhi ya tabia zetu huathiri afya zetu ikiwa ni pamoja na afya ya viungo vya uzazi na kupunguza au kuondoa uwezo wetu wa kuzaa watoto.ii}Bahati nzuri tabia hizi zinaweza kudhibitika._Chakula Na Mazoezi:_i} Ili tuwe na uwezo mzuri wa kuzaa watoto tunahitaji kupata chakula kizuri na kuipa miili yetu mazoezi ya kutosha.ii}Wanawake wenye unene wa kupindukia,uzito mdogo na mkubwa sana au tumbo kubwa wanakuwa miongoni mwa wenye matatizo hayaiii} _Uvutaji Wa Sigara_Uvutaji wa sigara unapunguza kiwango cha mbegu _(low sperm count)_ kwa wanaume, kuongeza uwezekano wa mimba kutoka,kuzaa mtoto mwenye uzito mdogo au kabla ya wakati _(njiti)_ kwa wanawake.iv} _Pombe:_-Unywaji wa pombe huongeza uwezekano wa kuzaa mtoto mwenye matatizo na unywaji uliozidi huweza kuleta ugonjwa, _Fetal Alcohol Syndrome_.-Kwa mwanaume,pombe hupunguza kiwango chake cha mbegu.v} _Madawa:_-Madawa kama bangi _(marijuana)_ hupunguza kiwango cha mbegu kwa wanaume.-Utumiaji wa cocaine kwa wanawake huathiri figo za watoto watakaozaliwa.
2.*Sababu Za Kimazingira*-Uwezo wa mwanamke kutunga mimba unaweza kuathiriwa na uwepo wake kwenye mazingira yenye sumu au kemikali.-Hii inaweza kuwa kwenye mazingira ya kazi au sehemu anayoishi.-Baadhi ya kemikali zilizobainika kupunguza uwezo wa mwanamke kupata mimba ni:1.*_Lead_*–husababisha mimba kutoka.2.*Tiba*-tiba ya mionzi ya mara kwa mara na *chemotherapy* huathiri uzalishaji wa mbegu za kiume na matatizo ya ovari.3*_Ethylene Oxide_*-kemikali inayotumika kuua wadudu kwenye vifaa vya upasuaji na kutengenza dawa za kuulia wadudu huleta dosari kwenye mimba changa na kusababisha mimba kutoka.*Dibromochloropropane (DBCP)*_– Kemikali inayopatikana kwenye dawa za kuulia wadudu husababisha mwanamke kukoma hedhi mapema.*DALILI ZA UGUMBA NA MATIBABU HUWA ZINAJULIKANA**DALILI KAMA*-Hedhi kupishana,-Hedhi kutoka kidogo sana,-Hedhi kutoka nyingi sana,-Maumivu makali ya tumbo wakati/kabla au baada ya hedhi-maumivu makali wakati wa tendo la ndoa-Kutokupata hedhi au hedhi kuruka miezi au kujirudia ndani ya mwezi ×2-kuhisi mara kwa mara hali ya ujauzito na kila ukipima ni negative -kutopata hamasa ya tendo la ndoa {si wote}*MATIBABU*-utatibiwa ugumba wewe mwanamke kulingana na chanzo cha tatizo kama tulivyo ona vyanzo kuwa ni vingi,-unashauriwa kutumia vyakula au virutubisho vya kusaidia hormon zako ziweze kubalance mara kwa mara-Kama una matatizo mojawapo kati ya hayo tulio jifunza iwe ni maumivu wakati wa hedhi,hedhi kupishana,hedhi kutoka kidogo,hedhi kutoka nyingi,hedhi kutoka chafu,maumivu wakati wa tendo unashauriwa kutafta ufumbuzi kabla,*USHAURI*-kumbuka kuna *primary infertility* na *secondary infertility* Nikimaanisha hata kama ulisha wahi kuwa na mtoto 1 au 2 nyuma bado unaweza ukapatwa na ugumba,cha muhimu niwewe kushughulikia dalili ulizo nazo.



1 comment:

Post Top Ad

Responsive Ads Here