Ujumbe kuhusu kinga na tiba yasaratani ya matiti - KABATA

This is the special room for news where you need to settle with!

Tuesday, 26 November 2019

Ujumbe kuhusu kinga na tiba yasaratani ya matiti

1. Fahamu visababishi • Kurithi • Umri mkubwa • Kupata mtoto wa kwanza baada ya umri wa miaka 35• Uzito mkubwa • Kutokufanya mazoezi • Matumizi ya tumbaku au pombe
. Fahamu hali ya kawaida kwakoFahamu hali ya kawaida ya matiti yako kwa kujitazama kwenye kioo au kujigusaUkigundua mabadiliko yoyote, nenda kituo cha kutolea huduma za afya kilicho karibu nawe  
3. Pata huduma za uchunguzi Huduma za uchunguzi unazoweza kufanyiwa ni pamoja na kipimo cha mamogramu, kutoa ute au kinyama (biopsy) kutoka katika uvimbe
4. Zingatia mtindo bora wa maisha ili kulinda afya yako• Zingatia uzito kulingana na ushauri wa mtaalamu wa afya • Fanya mazoezi ya mwili mara kwa mara • Punguza unywaji wa pombe Nyonyesha kwa kuzingatia ushauri wa wataalamu • Tumia matunda na mboga mboga kila siku • Epuka matumizi ya tumbaku
Mifano ya imani potofu zinazoenezwa mara nyingi Kuhusu Saratani ya Matiti Uvumi: Mionzi inayotolewa kwa ajili ya tiba ya saratani ya matiti\husababisha hatari zaidi kuliko manufaa. UKWELI: • Matibabu ya mionzi hutumika kuangamiza chembechembe za saratani. • Lengo la matibabu ya mionzi ni kuangamiza chembechembe za saratani zilizobakia ndani au karibu na titi baada ya upasuaji. • Matibabu ya mionzi yanaweza kusabisha athari ndogondogo ambazo huisha wiki chache baada ya kumaliza matibabu. • Mionzi ni njia muafaka wa kutibu saratani. Uvumi: Kama kuna historia ya saratani ya matiti katika familia, na mimi nitapata; kama hakuna historia mimi sitapata. UKWELI: • Wanawake wote wako katika hatari zaidi ya kupata saratani ya matiti. • Kuwa na ndugu mwenye Saratani ya matiti huongeza hatari ingawa si lazima upate. • Unaweza kuwa na Saratani ya matiti hata kama huna ndugu aliyewahi kupata ugonjwa huu. Uvumi: Saratani ya matiti mara zote huwa na uvimbe. UKWELI: • Mara nyingi saratani huwa na uvimbe; lakini mara nyingine saratani ya matiti hutokea bila uvimbe wowote. • Kuna dalili nyingine 7 zinazoweza kuashiria uwepo wa saratani ya matiti

Fahamu hali ya Kawaida KwakoDalili za saratani ya matiti hazifanani kwa wanawake wote. Ukigundua mabadiliko yoyote, nenda kituo cha afya kilicho karibu nawe. Fahamu hali ya Kawaida Kwako Imetayarishwa na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa Ushirikiano wa T-MARC Tanzania na Susan G. Komen. Habari hii imetolewa kwa kuzingatia kipengele Breast Self-Awareness Messages card for an African-American audience, mambari KO2003 9/15, Susan G. Komen®. Matumizi ya picha hizi hayaruhusiwi bila idhini iliyoandikwa kabla ya kutumika. Komen hatoi ushauri wa afya. 01/

No comments:

Post a Comment