Wagombea wa uenyekiti wa vijiji 126 kati ya 127 CCM wapita bila kupingwa wilayani Nachingwea - KABATA

This is the special room for news where you need to settle with!


Breaking

Friday, 15 November 2019

Wagombea wa uenyekiti wa vijiji 126 kati ya 127 CCM wapita bila kupingwa wilayani Nachingwea





Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi( CCM) 126 kati ya 127 katika vijiji 127 vya wilaya ya Nachingwea wamepita bila kupingwa katika nafasi ya uenyekiti wa serikali za vijiji.
Hayo yameelezwa leo na msimamizi wa uchaguzi wa wilaya ya Nachingwea, Nnunduma Ali alipozungumza na Muungwana Blog ndani ya ofisi yake iliyopo kwenye jengo la ofisi za halmashauri ya Nachingwea.
Nnunduma alisema CCM kimefanikiwa kushinda viti 126 kati ya viti 127 katika vijiji 127 vinavyounda wilaya ya Nachingwea baada ya baadhi ya wagombea wa vyama vya CUF na CHADEMA kuenguliwa kutokanana  kushindwa kukidhi vigezo.
Alisema  wanachama wa CCM walioteuliwa kugombea na fasi hizo ni 127. Hata hivyo nimgombea mmoja tu kati ya hao atapambana na mwanachama pekee wa CHADEMA aliyepitishwa kugombea nafasi hiyo.
Alisema kwa nafasi ya wenyeviti wa vijiji ni wana CCM 127 waliokuwa wamechukua , kurejesha fomu na kupitishwa kugombea, CHADEMA ni wanachama 52 pekee ambao walichukua,kurejesha fomu na mwanachama mmoja tu kati ya hao ndiye aliyepitishwa kugombea. Huku CUF hakuna mwanachama wake kati ya 12 waliochukua na kurejesha fomu za kuomba kuteuliwa kugombea.
Msimamizi huyo wa uchaguzi alisema licha ya chama hicho kupata ushindi wa mtemremko kwa nafasi ya uenyekiti wa vijiji, lakini pia kimekutana na bahati hiyo katika nafasi ya uenyekiti wa vitongoji. Baada ya wanachama wake 523 kupita bila kupingwe wakati Chama cha ADC kimefanikiwa kusimamisha wambea wanne. Wakati CUF na CHADEMA vikiambulia patupu kwakutokuwa na mgombea hata mmoja.
'' CCM katika nafasi za wajumbe mchanganyiko wanachama wake 1328 pia wamepita bila kupingwa. CUF kimefanikiwa kusimamisha wagombea 24 na CHADEMA wagombea 68. Ujumbe viti maalum CCM wagombea wake 904 kati ya 1016 wamepita bila kupingwa, CUF kimesimamisha wagombea 13 na CHADEMA 39 ndio walioteuliwa kuwania nafasi hizo,'' alisema Nnunduma.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here