Wana SACCOS walia na mamilioni yao yaliyo mikononi mwa watu - KABATA

This is the special room for news where you need to settle with!


Breaking

Tuesday, 5 November 2019

Wana SACCOS walia na mamilioni yao yaliyo mikononi mwa watu





Zaidi ya fedha zinazopindukia milioni 200 za chama cha Ushirika cha Igoma Saccos halmashauri ya mji wa Njombe mkoani Njombe,zipo mikononi mwa wanachama wake ambao wamekopa na mpaka hivi sasa hazijarejeshwa na hivyo kukiweka chama hicho katika hali mbaya Ya kufilisika kutokana na baadhi ya wanachama kukopa fedha na kushindwa kuzirejesha kwa wakati.




Desius Mwageni ni Mwenyekiti wa Igoma Saccos anathibitisha juu ya Usugu wa Madeni katika Saccos hiyo ambayo kwa sasa inatajwa kuwa katika Hali mbaya ya kufilisika kutokana na Ukosefu wa Uaminifu wa Wanachama ambao wamekopa fedha zaidi ya miaka mitatu Nyuma na Kushindwa kuziresha mpaka hivi leo na hivyo kufifisha uwezo wa Saccos hiyo kujiendesha.Aidha Bw. Desius amemshukuru mkuu wa mkoa wa Njombe Christopher Ole sendeka kwa agizo lake la kuwataka  wote wanaodaiwa na vyama mbalimbali vya Ushirika kikiwemo chama cha Igoma Saccos kulejesha fedha hizo ,Ambapo amesema kuwa kauli hiyo itahamasisha wadaiwa Sugu kujisarimisha kabla ya mkono wa sheria kuanza kufanya kazi hapo tarehe 11 Mwezi Desember Mwaka huu.


"Watu ni wazembe kulipa mikopo halafu pia ukifuatilia wanaleta matatizo hawatii amri za viongozi,na changamoto ukifuatilia sana ni uchumi ndio tatizo,rasimali zao ukiendelea kufuatilia haziuziki na mpaka mwezi wa tisa ni milioni kama 200 nawadai mpaka kwenye chama tumeingia hasra kubwa"alisema Mwenyekiti

Baadhi ya wanachama wa Saccos hiyo wanakiri kuwa Miongoni mwao wapo wadaiwa sugu ambao hawataki kuresha fedha hizo ili hali mda wa marejeshio ushaisha na hivyo kumtaka mwenyekiti wa Saccos hiyo kuwa mkali zaidi ili fedha hizo Zirejee katika mzunguko wa Saccos hiyo.

Exzaud Sapali ni kaimu mrajisi mkoa wa Njombe amewataka wanachama wa Saccos hiyo kurejesha mikopo hiyo kabla ya wiki mbili ya agizo la mkuu wa mkoa.

"Kwa kweli lazima tuwe wakali,watu mmechukuwa fedha hamtaki kurejesha,naomba nisisitize kauli ya mh.Mkuu wa mkoa fedha mlizo zichukuwa za Saccos hii mzirejeshe kulingana na mda uliotolewa na mkuu wa mkoa"alisema Sapali

Tarehe 24 mwezi wa 10 mkuu wa mkoa wa Njombe Cristopher Ole sendeka alizungumza na baadhi ya viongozi wa vyama vya ushirika na wadaiwa sugu ambapo aliagiza ifikapo tarehe 11 mwezi wa 12 kila mdaiwa awe amelipa fedha alizokopa katika vyama vya ushirika.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here