This is the special room for news where you need to settle with!
Watoa huduma wa afya wameaswa kuzingatia uadilifu na uaminifu mahala pa kazi kwa kutokuomba wala kupokea rushwa wakati wa kutoa huduma.
“Kupokea zawadi au pesa kabla na baada ya kutoa huduma ni kosa kisheria na pindiutakapogundulika umefanya hivyo basi utachukuliwa hatua kulingana na vifungu 24 vya makosa ya rushwa vilivyoainishwa katika sheria namba 11 ya mwaka 2007 ya kuzuia na kupambana na rushwa,” Amesema Bi. Majule.
Kwa upande wake Muuguzi katika Hospitali ya Mloganzila, Bw. Mosama John ametoa wito kwa wataalam hao kuwa na kauli nzuri wakati wa kuwahudumia wateja wanaokuja hospitalini hapa kwa ajili ya kupatiwa matibabu.
No comments:
Post a Comment