Wazee wa CCM waridhishwa na utendaji kazi wa Rais Dk. Shein - KABATA

This is the special room for news where you need to settle with!


Breaking

Sunday, 17 November 2019

Wazee wa CCM waridhishwa na utendaji kazi wa Rais Dk. Shein


Wazee wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Dimani Kichama wameeleza kuridhishwa na uongozi wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein ambaye pia, ni Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na kukiri kwamba anawatendea haki.
Wazee hao wa CCM, Wilaya ya Dimani Kichama waliyasema hayo leo huko katika ukumbi wa Afisi ya CCM Mkoa wa Mjini iliyopo Amani, Mkoa wa Mjini Magharibi katika Mkutano aliouandaa Rais Dk. Shein ambaye pia ni Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar kwa ajili ya wazee hao ikiwa ni muendelezo wa mikutano hiyo iliyoanza jana hapa Unguja ambapo tayari kwa upande wa kisiwani Pemba imeshafanyika.
Katika hotuba yao wazee hao walikiri kuwa Rais Dk. Shein katika kipindi chake cha uongozi wa Awamu ya Saba amekuwa akiwatendelea haki katika kuleta maendeleo huku akiwa anasimamia vyema utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015-2020 sambamba na kustawisha huduma za jamii.
Walieleza kuwa katika Wilaya yao wamefaidika kwa mambo makubwa mno kama vile huduma za elimu bure ambapo tayri katika Wilaya yao wana skuli 6 za Ghorofa za Sekondari hivi sasa, huduma za miundombinu ambapo tayari kero za barabara ya Kibondemzungu na Mwanakwerekwe zimeshatatuka na hivi sasa zinapitika.



No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here