Waziri Mkuu awapa ushauri wasanii kuhusu Baba wa Taifa - KABATA

This is the special room for news where you need to settle with!


Breaking

Friday, 15 November 2019

Waziri Mkuu awapa ushauri wasanii kuhusu Baba wa Taifa



Waziri mkuu, Kassim Majaliwa amewashauri wasanii nchini kuboresha Tamasha la Sanaa la Mwl. Nyerere kwa kuandaa maonesho maalum ya kazi zao wanazofanya nchini sambamba na kujitangaza kimataifa.
Amesema hayo wakati wa kuzindua Tamasha la Mwl. Nyerere lililohudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo Spika wa Bunge, Job Ndugai, tamasha linalofanyika kwenye ukumbi wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es salaaam.
Waziri mkuu amesema, kwa mwaka huu amefurahishwa na wazo hilo lakini angefurahi zaidi kuona tamasha hilo linaandaliwa mapema huku likiambatana na maonesho ya kazi za sanaa.
“Uamuzi wenu wa kuandaa tamasha hili ni wa Kizalendo, na unaakisi nia yenu thabiti ya kuunga mkono jitihada zinazoendana na shughuli ambazo Baba wa Taifa alizifanya wakati wa uhai wake na kuwa fundisho kwetu sote”, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.
Katika Tamasha hilo pia, wasanii hao wamezindua mfuko ambao utawasaidia katika kuwainua kimaisha na kupitia harambee iliyoendeshwa na waziri mkuu, zaidi ya shilingi milioni 140 zimepatikana huku Rais John Magufuli akichangia shilingi milioni 100.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here