Boris Johnson aapishwa rasmi kuwa Waziri Mkuu wa Uingereza - KABATA

This is the special room for news where you need to settle with!


Breaking

Monday, 16 December 2019

Boris Johnson aapishwa rasmi kuwa Waziri Mkuu wa Uingereza


Kiongozi wa Chama cha Kihafidhina cha Uingereza Bw. Boris Johnson jana aliapishwa rasmi kuwa waziri mkuu wa Uingereza baada ya kushinda kwenye uchaguzi wa Baraza la chini la bunge la Uingereza.
Kwenye hotuba aliyotoa jana baada ya ushindi Bw. Johnson alisema Uingereza imetandika njia na kumaliza mvutano na kukaribisha zama mpya. Amesisitiza kuwa Uingereza itajitoa rasmi kwenye Umoja wa Ulaya tarehe 31 mwezi ujao.
Wakati huohuo, mkutano wa kilele wa siku mbili wa Umoja wa Ulaya ulikamilika jana mjini Brussels, ambapo viongozi wa umoja huo walijadili juu ya masuala ya Brexit, Makubaliano ya Umoja wa Ulaya ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi, na mageuzi ya Shirika la Biashara Duniani. Pia wamehimiza Uingereza kuidhinisha na kutekeleza makubaliano ya Brexit haraka iwezekanavyo.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here