Kikundi cha kwaya ya Barabara ya 13 Ulyankulu Tabora - KABATA

This is the special room for news where you need to settle with!


Breaking

Tuesday, 24 December 2019

Kikundi cha kwaya ya Barabara ya 13 Ulyankulu Tabora



Kwaya maarufu ya Kanisa la FPCT, Ulyankulu, Urambo Tabora, iliyowahi kutamba katika medani za muziki wa Injili katika miaka ya 80, inayojulikana kwa jina la Ulyankulu Barabara 13, ilifanya uzinduzi wa albam mbili kwa mpigo, kwenye ukumbi wa BCIC HALL MBEZI BEACH katika maeneo ya Interchick Jijini Dar es Salaam.

Akiongea na mwandishi wa habari hii kiongozi wa Kanisa hilo Mch. Joseph Malumbu, aliyeongozana na kwaya hiyo alisema kwaya hiyo itazindua kwanza albam yenye nyimbo 13, mpya ambazo baadhi yake hazijawahi kusikika masikioni mwa wasikilizaji, zilizorekodiwa katika mkanda wa kawaida (Audio) na katika CD kabla ya kuzindua albam yenye nyimbo 10, Mchanganyiko watakazo zikusanya kutoka katika albam zao mbali mbali walizorekodi ambazo zitarekodiwa katika VHS, Audio, CD na DVD.

Alisema albam zinazozinduliwa ni ya 7 na 8 na kuongeza kuwa wameamua kuzindua zote kwa pamoja kutokana na zote kuhitajika kwa wakati mmoja hasa kwa wakazi wa jiji la Dar es Salaam ambao zaidi walipenda kuziona nyimbo hizo ambazo awali walikuwa wakizikia redioni tu.

Mchungaji huyo eliendelea kusema kuwa pamoja na yote hayo lakini kikubwa ilikuwa ni kuondoa Kiu ya wakazi wa Dar es Salaam ikiwa ni pamoja na kuondoa uzushi wa baadhi ya watu wasioitakia mema kwaya yao baada ya kuvumisha kuwa baadhi ya watu muhimu katika kwaya hiyo wamefariki dunia wakiacha kundi likisambaratika.


Naye Mwenyekiti wa kwaya hiyo Bw. Peter Nyandwi, aliwaondoa wasiwasi wale wote wanaodhani kuwa kwaya yao ina nyimbo za kizamani pekee waje kwa wingi kwa kuwa kwaya hiyo inazo nyimbo nyingi zinazokwenda na wakati ambazo anaamini zitapendwa na watu wa rika zote.

Wakizitaja nyimbo zilizopo katika albam ya nyimbo mchanganyiko itakayorekodiwa pia katika mkanda wa VHS viongozi wa kwaya hiyo walisema ni pamoja na Dunia ya shida, Esau, Tunakumbuka kifo, Nikifikiria, ulinikimbia, Yusufu, nitamuona Yesu, Basi nasema, ufunuo wa Yohana na Samsoni na Delila Uliobeba albam.

Kabla ya kikundi hiki kuimba ukumbini BCIC, pia walizindua katika ukumbi wa PTA HALL SABSABA ambapo Mgeni rasmi katika uzinduzi huo alikuwa ni Naibu Meja wa Majiji ya Afrika, Mhe Hanzuruni Mungulu wakati kwaya zinazopamba uzinduzi ni Lulu Mtoni, Dovya Gospel Singers, Unity Group na waimbaji binafsi ni Christina Shusho, Amoni na Upendo Kilahiro na wengine Wengi.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here