Serikali kukata rufaa tena kesi dhidi ya Abdul Nondo - KABATA

This is the special room for news where you need to settle with!


Breaking

Friday, 27 December 2019

Serikali kukata rufaa tena kesi dhidi ya Abdul Nondo




Serikali imepanga kukata rufaa dhidi ya aliyekuwa Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi Tanzania (TSNP), Abdul Nondo, ikiwa ni baada ya Mahakama Kuu ya Iringa kumpa ushindi katika rufaa iliyokuwa imekatwa na Serikali na hakaonekana kuwa hana hatia.
Notisi hiyo imewasilishwa mahakama ya Rufaa kanda ya Iringa tarehe 24.12.2019 siku moja baada ya hukumu kutolewa.
Itakumbukwa kwamba Nondo alishtakiwa kwa kosa la kutoa taarifa za uongo kinyume na kifungu cha 16 cha Sheria ya Makosa ya Kimtandao ambapo mahakama ya Wilaya Iringa ilimkuta hana hatia, kisha maamuzi hayo kukatiwa rufaa mahakama kuu ambapo Jaji Kente naye pia aliamua kuwa Nondo hana hatia kwakuwa upande wa Jamhuri ulishindwa kuthibitisha vinginevyo.


No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here