Monday, 30 December 2019
Ugonjwa wa Tete Kuwanga (Chicken Pox)
Tete kuwanga ni ugonjwa ambao unaombukiza na kusababishwa na virusi vinavyojulikana kama Varicella zoster virus.Maambukizi ya tete kuwanga huonekana sana kwa watoto wadogo ingawa hata watu wakubwa pia hupata maambukizi ya ugonjwa huu. Tete kuwanga hupatikana duniani kote.Katika nchi zenye kupata majira ya baridi, maambukizi ya ugonjwa huu huonekana sana wakati wa kipindi cha majira ya baridi na kipindi cha masika. Watoto walio na umri wa miaka 4-6 wako kwenye hatari kubwa ya kupata maambukizi ya tete kuwanga na ndio katika umri huu ambapo maambukizi ya ugonjwa huu yapo kwenye kiwango cha juu sana.Inakadiriwa ya kwamba, tete kuwanga huambukiza kwa kiwango cha asilimia 90. Watoto wengi hupata maambukizi ya tete kuwanga kabla ya kufikia umri wa kubaleghe ingawa asilimia 10 ya vijana bado wanakuwa kwenye hatari ya kupata maambukizi ya tete kuwanga. Katika nchi za tropiki,maambukizi ya tete kuwanga huonekana kwa watu wakubwa na huenda yakawa maambukizi ya hatari sana.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Responsive Ads Here
Author Details
Templatesyard is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of templatesyard is to provide the best quality blogger templates which are professionally designed and perfectlly seo optimized to deliver best result for your blog.

No comments:
Post a Comment