Watatu washikiliwa na Polisi kwa tuhuma za mauaji - KABATA

This is the special room for news where you need to settle with!


Breaking

Friday, 6 December 2019

Watatu washikiliwa na Polisi kwa tuhuma za mauaji


Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linawashikilia watu watatu kwa tuhuma za mauaji ya mtu mmoja aliyetambulika kwa jina la John Lubisi Mwakarundwa (62) mkazi wa Kitumba.
Inadaiwa kuwa mnamo Disemba 3, 2019 majira ya saa 17:15 jioni huko Kitongoji cha Kitumba, Kijiji na Kata ya Nkunga, Tarafa ya Ukukwe, Wilaya ya Rungwe, Mkoa wa Mbeya, watu hao walimuua John  kwa kumkata na kitu chenye ncha kali sehemu za kisogoni, taya la kushoto na tumboni.
Mwili wa marehemu umehifadhiwa Hospitali ya Makandana – Tukuyu.
Taarifa ya Jeshi la Polisi mkoani humo inasema upelelezi wa shauri hilo unaendelea na mara baada ya kukamilika, watuhumiwa watafikishwa Mahakamani kwa hatua zaidi za kisheria.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here