Watoto 56 wafanyiwa upasuaji wa Moyo kambi maalum JKCI - KABATA

This is the special room for news where you need to settle with!


Breaking

Friday, 6 December 2019

Watoto 56 wafanyiwa upasuaji wa Moyo kambi maalum JKCI


Madaktari bingwa wa magonjwa ya moyo kwa watoto wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na wenzao kutoka  King Salman Humanitarian Aid and Relief Center wa nchini Saud Arabia wakimfanyia upasuaji wa bila kufungua kifua na kuziba tundu la moyo wa mtoto kwa kutumia mtambo wa Cathlab wakati wa kambi maalum ya matibabu inayofanyika katika Taasisi hiyo.
Jumla ya watoto 33 wamefanyiwa upasuaji mdogo wa bila kufungua kifua ambapo hali zao zinaendelea vizuri na wengine wameruhusiwa kurudi nyumbani.
Madaktari bingwa wa magonjwa ya moyo kwa watoto wa JKCI kwa kushirikiana na  wenzao kutoka  King Salman Humanitarian Aid and Relief Center wa nchini Saud Arabia wakimfanyia  mtoto upasuaji mkubwa wa kusimamisha moyo na kurekebisha mishipa ya damu ya moyo  katika  kambi maalum ya matibabu inayoendelea katika Taasisi hiyo.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here