Z>ao la embe hustawi vizuri katika maeneo ya tambarare na miinuko kati ya
futi 0-600 usawa wa bahari. Kiwango cha wastani cha mvua inayohitajika kwa
kilimo cha embe ni mililita 650 hadi 1850 kwa mwaka. Miembe hustawi katika
udongo wenye uchachu (ph) kati ya 5.5 na 7.2. udongo wenye chachu Zaidi huwa
na upungufu wa madini mbalimbali ikiwemo Zinki, Chuma, Fosforas na Kalsham.
Kuandaa mashimo Kuchimba mashimo mapana kutafanya udongo uwe laini ili
kusaidia mizizi kuzaliwa kwa wingi, upana wa shimo uwe sentimita 60x60 upana
kwa urefu, kwa maeneo yenye udongo mgumu na miamba ya mawe kipimo kiwe
sentimita 100x100 upana na urefu. Uchimbaji wa mashimo uwe wa kutengeneza
udongo katika sehemu mbili. Sehemu ya kwanza ni udongo wa juu wa kina cha
sentimita 30 na sehemu ya pili ni udongo sentimita zilizobaki za kina cha
shimo. Mbolea. Tumia mbolea samadi au mboji iliyoiva vizuri debe moja hadi
mbili kwa shimo, changaya mbole na udongo wa kwanza kutoka shimoni, iwapo
itatumika mbolea ya viwandani kama DAP, TSP, NPK au Minjingu Phosphate
changanya mbolea hiyo na udongo wa juu wenye mboji (top soil). Upandaji.
Panda miche ya miembe katika misimi ya mvua za mwaka, au wakati wowote iwapo
inatumika njia ya umwagiliaji kwa vipindi visivyo na mvua. Weka maji ya
kutosha wakati wa upandaji ili kuimarisha mshikamano wa udongo na unyevu.
Vipimo. Miembe hupandwa katika vipimo tofauti kutegemeana mipango ya
matumizi ya ardhi husika na miundombinu ya shamba. Upandaji unaweza kuwa wa
miti 160 hadi 1300 kwa hekta moja. Vipimo vya umbali kati ya mti ana mti
vifuate mistari iliyonyooka. Kipimo cha wastani kwa wakulima wadogo na
wakati ni mita 8x8, mita 6x8, mita 4x8, mita 4x7 au mita 5x7. Wastani kwa
hekta ni miembe 200-400 ujazo wa vipimo vingine vinaweza kufikia miti 1200
na Zaidi kwa hekta. Matumizi kwa vipimi hivyo vinahitaji ushauri wa mtaala,
kabla ya kutumia. Ukatiaji. Ukatiaji hufanyika katika hatua ya kwanza ya
ukuaji miti ukifikia urefu wa sentimiti 60-100, ukatiaji wa kwanza
utatofatiana na ukatiaji wa pili na kuendelea. Ukatiaji wa kwanza, kata
sehemu majani yanapopishana ili kupata umbo la mti unaopishana kutoka katika
chanzo cha tofauti. Ukatiaji wa pili na kuendelea kata sehemu ya juu ya
pingili ya tawi ili kupata matawi mengi. Magonjwa na wadudu. Miembe
hushambuliwa na magonjwa kama Ubwiru unga (powder mildew), Chule
(Antharacnose), magonjwa mengine hutokea kwa mara chache sana. Wadudu
mbalimbali wanaoshambulia mazao tofauti, hushambulia miti ya miembe kama
Vidukari, Vung’ata, Kifaurongo, Mbawa kavu, nk. Udhibiti wa magonjwa na
wadudu. Fanya usafi wa palizi shambani kila inapolazimu ili kupnguza vyanzo
wa wadudu na magonjwa, matumizi ya dawa yanafanyika kila dalili za ugonjwa
zaitakapo jitokeza au mashambulizi ya wadudu yatakapoonekana. Ukatiaji
mkubwa. Miembe inapokuwa katika hatua ya uzalishaji huhitaji kukatiwa kila
imaliziapo hatua ya uvunaji na kujiandaa kwa uzalishaji katika msimu ujao.
Ukatiaji huu huwezesha mti kuchipua majani mapya kwa pamoja na kukomaa kwa
pamoja, hatimae hutoa maua kwa pamoja kwa wakati unaokusudiwa. Urutubishaji
na mbolea. Mbolea ni muhimu katika uzalishaji wa embe, mbolea huendelea
kutumika wakati wa kukuza miche na kuzalisha matunda. Mbolea zinazotumika ni
N.PK, MOP, Urea, Minjingu, Samadi, Mboji, Chokaa na virutubisho visaidizi.
Mbolea zitawekwa kulingana na mahitaji ya udongo na kwa wakati maalum,
uwekaji holela wa mbolea unaweza ukaathiri uzalishaji utakaotokana na
ukosefu wa maua. Uvunaji na uhifadhi Embe zitunzwe zikiwa zimekomaa, embe
lililokomaa lina umbo tofauti kulingana na aina ya embe, kiashiria kikuu ni
embe kubonya kwa eneo la kikonyo, alama nyingine ni kubadilika kwa rangi ya
ndani ya nyama ya embe kutoka nyeupe kuwa njano hafifu. Embe zinazovunwa
zioshewe kwa maji ya moto na kuhifadhiwa sehemu kavu na salama, chagua embe
na kuziweka katika madaraja mfano daraja la 1 na daraja 2. Hii itakusaidia
kujua ipi embe ni tayari kwa kupeleka sokoni.
Friday, 16 April 2021
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Responsive Ads Here
Author Details
Templatesyard is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of templatesyard is to provide the best quality blogger templates which are professionally designed and perfectlly seo optimized to deliver best result for your blog.
No comments:
Post a Comment