CCM kumpeleka Zitto mahakamani ikidai kudhalilishwa - KABATA

This is the special room for news where you need to settle with!


Breaking

Sunday, 16 May 2021

CCM kumpeleka Zitto mahakamani ikidai kudhalilishwa

 

Baada ya kiongozi ACT Wazalendo, Zitto Kabwe kudai kuvamiwa na gari tatu za CCM, Katibu wa chama hicho tawala Mkoa wa Kigoma, Kajoro Vyohoroka amesema wanasubiria matokeo yatangazwe wafungue jalada mahakamani la kudhalilishwa na kiongozi huyo.


"Sisi kwenye kampeni tulikuwa na magari 48 katika Jimbo la Muhambwe pekee sawa na gari mbili kila kata sasa yeye kaona magari yanapita kwenye vituo huko akaanza kusambaza taarifa yanasambaza kura bandia tutamchukulia hatua baada ya matokeo kutangazwa," amesema Vyohoroka.


Mwenyekiti huyo wa ACT Wazalendo alituma ujumbe mfupi kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter uliosomeka," tumetoka polisi. OCD wa Kibondo ametusaidia sana. Tupo salama. Tunaendelea kulinda ushindi wetu hapa Muhambwe mpaka mwisho. Polisi wamefanya kazi kwa weledi kabisa. Ni hatua kubwa.”

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here