Herbeauty Mbunge Nusrat Hanje ahoji Darasa la 7 kukosa ajira serikalini - KABATA

This is the special room for news where you need to settle with!


Breaking

Thursday, 27 May 2021

Herbeauty Mbunge Nusrat Hanje ahoji Darasa la 7 kukosa ajira serikalini

Mbunge wa Viti Maalum Nusrat Hanje, amehoji ni kwanini vijana waliomaliza darasa la saba hawapewi fursa ya kuajiriwa na taasisi za serikali hata kama wanazo fani walizozipata kupitia vyuo vya ufundi vinavyotambulika na serikali kwa kigezo cha kutokuwa na cheti cha kidato cha nne.

Kauli ameitoa Bungeni hii leo Mei 27, 2021, wakati akiuliza swali kwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, na kuiomba serikali iangalie namna ya kuwaajiri kwani hivyo vyuo vinatambulika, ambapo Waziri Mkuu alijibu kwamba tatizo la ajira ni la Dunia nzima hivyo serikali inao mkakati wa kuanzisha viwanda vitakavyoweza kutoa ajira kwa watu wote.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here