India imetoa shukrani za dhati kwa Uturuki kwa kutuma misaada ya Covid-19.
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya India Arindam Bagchi, alisema kuwa wanakaribisha "ishara ya mshikamano" wa Uturuki na kushukuru Shirika la Hilali Nyekundu la Uturuki kwa msaada.
Sanjay Kumar Panda, Balozi wa India huko Ankara, alisisitiza kuwa vifaa vya matibabu ni "muhimu" kwa nchi yake, katika ujumbe aliochapisha kwenye akaunti yake ya Twitter ambapo alisema,
"Ninashukuru Uturuki kwa kuwa pamoja na India katika kipindi hiki kigumu."
Shirika la Hilali Nyekundu la Uturuki liliwasilisha ndege mbili za mizigo zilizojaa vifaa vya matibabu kwa Shirika la Msalaba Mwekundu la India kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Indira Gandhi ili kusaidia watu wa India walioathiriwa na janga la Covid-19.
Miongoni mwa misaada hiyo, kulikuwa na mitungi 630 ya oksijeni, jenereta 5 za oksijeni, vifaa 50 vya kupumulia, dawa elfu 50 na vifaa anuwai vya matibabu vilivyoandaliwa na Shirika la Hilali Nyekundu la Uturuki pamoja na Wizara ya Afya.
No comments:
Post a Comment