Mrisho Gambo ataka wafanyakazi viwanja vya ndege kuvaa barakoa - KABATA

This is the special room for news where you need to settle with!


Breaking

Tuesday, 18 May 2021

Mrisho Gambo ataka wafanyakazi viwanja vya ndege kuvaa barakoa

 




Mbunge wa Arusha Mjini (CCM), Mrisho Gambo amesema ni imani yake wafanyakazi wa mamlaka za viwanja vya ndege wataanza kuchukua hatua za kujikinga na ugonjwa wa Covid-19 unaosababishwa na virusi vya corona baada ya ripoti iliyotolewa jana kwa  Serikali.

Jana Jumatatu Mei 17, 2021 kamati ya tathmini ya ugonjwa huo iliishauri Serikali kuendelea na hatua kuelekea kuruhusu matumizi huru ya chanjo dhidi ya ugonjwa huo

Kamati hiyo iliundwa na Rais Samia Suluhu Hassan ili kufanya tathmini na kuishauri Serikali hatua za kitaalamu za kufuata ili kukabiliana na ugonjw ahuo

Akizungumza bungeni leo Jumanne Mei 18, 2021 wakati akichangia makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi 2021/22, Gambo amesema ni imani yake kuwa wafanyakazi wa mamlaka za viwanja vya ndege nchini wataanza kuvaa barakoa na vifaa vingine vitakavyoionyesha dunia kuwa Tanzania ipo makini na jambo hilo.

Amedai hali hiyo itafanya watalii wengi zaidi wafike nchini na Serikali itaendelea kupata mapato kupitia sekta ya utalii, “ili watalii waje wengi zaidi tuendelee kupata dola na miradi hii tunayoiongea leo iweze kufanyiwa kazi.”

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here