Rais Samia azindua Kiwanda cha ushonaji cha Jeshi la Polisi - KABATA

This is the special room for news where you need to settle with!


Breaking

Tuesday, 18 May 2021

Rais Samia azindua Kiwanda cha ushonaji cha Jeshi la Polisi

 


Rais Samia Suluhu Hassan amezindua kiwanda cha ushonaji cha Jeshi la Polisi kilichopo Kurasini mkoani Dar es salaam, ambacho kitakuwa kikishona sare za askari wa jeshi hilo.

Kiwanda hicho ambacho ni cha kisasa kitakuwa na uwezo wa kushona sare mia nane kwa siku kutoka sare mia mbili za askari polisi zilizokuwa zikishonwa hapo awali.

Zaidi ya shilingi milioni mia sita zimetumika katika ujenzi wa kiwanda hicho, ujenzi ulioanza mwezi June mwaka 2020.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here