Waandishi wa habari wajengewa uwezo kuripoti kwa usahihi tatizo la Sumu kuvu - KABATA

This is the special room for news where you need to settle with!


Breaking

Tuesday, 18 May 2021

Waandishi wa habari wajengewa uwezo kuripoti kwa usahihi tatizo la Sumu kuvu

 



Katika kuhakikisha inapanua wigo wa uelewa na kuripoti kwa usahihi kwa jamii juu ya madhara  yatokanayo na sumu kuvu Wizara ya Kilimo kupitia mradi wa kudhibiti sumu kuvu TANPAC imeanza kutoa elimu kwa waandishi wa habari namna ya kuripoti na kutoa elimu juu ya tatizo la sumu kuvu.

Semina hiyo inalenga kumpa mwandishi uelewa mpana ambaye yeye atakuwa kiungo baina ya Jamii lakini pia Serikali katika kudhibiti na kuzuia tatizo la  sumu kuvu. 

Akizungumza  wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Usalama na chakula Josephine Yamondo amesema Wizara ya kilimo iliandaa mradi ambao ulizinduliwa  mwaka 2019 na kuanza kufanya kazi 2020.

Amesema mradi wa Sumukuvu ulitambuliwa baada ya kugundua  madhara kwa wananchi yamekithiri ambapo serikali ikazindua mradi wa kudhibiti uchafuzi wa Sumukuvu katika Usalama wa chakula.

" Tumewapeni Mafunzo nyinyi wanahabari kwasabau nauwezo Mkubwa wa kufikia jamii kwa haraka hivyo mafunzo haya kwenu ni njia mojawapo ya kwenda kuhabarisha jamii juu ya uchafuzi wa Sumukuvu na athari zake kwenye chakula na kuondoa taharuki," amesema

Ameeleza kuwa Sumukuvu inaleta hofu katika jamii hivyo mkawe mstari wa mbele katika kuwaelimidha jamii juu ya Sumukuvu na tuondoe tahariki katika jamii kwani sumukuvu ilikuwepo yangu hapo zamani," amesema Yamondo

Kwa Upande wake, Mwanaidi Kiya kutoka Wizara ya kilimo Kitengo Cha Usalama na Uhakika wa chakula amesema Takwimu kutoka Shirika la Chakula Duniani (WHO) zinasema kwamba mtu mmoja Kati ya Watu 10 wanakufa kila mwaka kutokana uchafuzi wa chakula.

Ni hapa ambapo amsema  kila mwaka Bilioni 110 zinapotea kwenye Kilimo na Takwimu hizo zenaonekana kwenye nchi za kipato Cha chini na zakati kama Tanzania

" Kwa hali hiyo tutashindwa kuendeleza shughuli za Kilimo kwani tumekuwa tukipoteza pesa nyingi," amesema Kiya.

Nae mtafiti Mkuu Wizara ya kilimo Dkt Analice Kamala amesema Sumukuvu tangia zamani ambapo wengi waliathilika kwa kupata ulemavu wa viungo jambo lilioitwa nalaana.

Vilevile ametaja aina 400 za Sumukuvu zilizovumbuliwa na wataalamu wa afya ambapo chakula kinaweza kuwa na Sumukuvu kama Mkulima hakuzingatia sheria za utaratibu wa Kilimo mwanzo Kilimo mpaka Mwisho wa mavuno.

Hata hivyo amesema Chakula kinaweza kisiwe Salama  kipindi Cha mazao yanapokuwa shambani, kipindi Cha mavuno,kipindi Cha mauzo na kipindi Cha udafirishaji kama tu Mkulima hata tumia utaratibu hukika wa Kilimo hautofuatwa.

Madhara ya Sumukuvu yanaweza kujitokeza  ndani ya muda mfupi au muda mrefu na itategemea ni kiasi gani Cha chakula kilicholiwa.

Pia amewataja Watu walipo hatarini kuathiriwa na Sumukuvu nipamoja na watoto walio chini ya Mika mitano kupata udumavu ,wagonjwa kutokana na kingazao za mwili kuwa chini,wazee na wamama wajawaziti.

Wizara ya kilimo unatekeleza mradi wa kudhibiti Sumukuvu hapa Nchini kwa lengo la kuimarisha Usalama wa chakula na kuboresha afya ya wananchi katika uelimusha jamii kwa kutumia Vyombo vya habari.

 

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here