Iraq yaomboleza vifo vya watu 36 - KABATA

This is the special room for news where you need to settle with!

Wednesday, 21 July 2021

Iraq yaomboleza vifo vya watu 36

 


Iraq inaomboleza vifo vya watu 36 waliouawa kwenye shambulio la bomu katika soko lenye shughuli nyingi mjini Baghdad. 


Kundi la kigaidi linalojiita Dola la Kiislamu-IS limedai kuhusika- na shambulio hilo la leo.Hakuna idadi rasmi ya vifo iliyotolewa na maafisa wa Iraq lakini vyanzo vya matibabu vimeliambia shirika la habari la AFP Kuwa watu wasiopungua 36 wameuawa na wengine 60 wamejeruhiwa. 


Shambulio hilo ambalo linatajwa kuwa baya zaidi kutokea katika miaka ya hivi karibuni nchini humo, limegharimu maisha ya wanawake wengi na watoto siku moja tu kabla ya maadhimisho ya sikukuu ya Eid-al Adha.


Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Iraq umesema shambulio hilo linaonyesha kuwa ugaidi haujui mipaka, wakati ubalozi wa Ujerumani ukielezea kuskitishwa kwake na shambulio hilo la kinyama.


No comments:

Post a Comment