Bodi ya Shirika la Fedha Duniani (IMF) imeidhinisha dola milioni 567 kama mpango wa dharura kuisaidia Tanzania katika kampeni yake ya utoaji chanjo dhidi ya COVID-19.
Kwenye taarifa, shirika hilo limesema kitita hicho pia kitasaidia kugharamia mahitaji ya kiafya na kijamii kutokana na janga la virusi vya corona.
IMF imesema Tanzania inahitaji kiwango cha fedha sawa na asilimia 1.5 ya pato jumla la nchi, mnamo wakati mamlaka zikiweka mpango kabambe wa kushughulikia athari za janga hilo ambalo limeingia wimbi la tatu nchini humo.
Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa IMF Bo Li, amesema Tanzania inahitaji msaada wa kifedha kwa dharura na akiongeza kuwa mipango yake ya kampeni za utoaji chanjo na kugharamia huduma za afya na jamii itasaidia kudhibiti janga hilo.
Mripuko wa ugonjwa wa COVID-19 pamoja na marufuku ya usafiri, vimesababisha sekta ya utalii kuporomoka katika taifa hilo la Afrika mashariki.

No comments:
Post a Comment