Baerbock atarajiwa kuwa waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani - KABATA

This is the special room for news where you need to settle with!


Breaking

Friday, 26 November 2021

Baerbock atarajiwa kuwa waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani

 


Kiongozi mwenza wa Chama cha kijani cha Ujerumani Annalena Baerbock, anatarajiwa kuwa waziri wa kwanza mwanamke wa mambo ya nje katika serikali ijayo. 

Chama hicho pia kimemthibitisha kiongozi mwenza Robert Habeck kushikilia wadhifa wa makamu Kansela na wizara itakayoshughulikia uchumi, nishati na ulinzi wa mazingira. 

Uteuzi huo, pamoja na ule wa nyadhifa nyingine za baraza la mawaziri, umefanyika siku ya Alhamisi mwanzoni mwa mchakato wa mashauriano na wanachama wa chama cha kijani, ili kuridhia makubaliano ya muungano yaliyofikiwa baina yake na vyama vya Social Democrats (SPD) na Free Democrats (FDP).

Baerbock mwenye umri wa miaka 40 anatarajiwa kuanza majukumu yake mwanzoni mwa mwezi ujao mara tu baada ya serikali mpya ya vyama vitatu kuundwa rasmi.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here