Chama cha Madaktari cha Afrika Kusini (SAMA) kimesema watu ambao wamepata maambukizo ya aina mpya ya virusi vya Covid-19 ya Omicron nchini humo hawajaugua kwa kiwango kikubwa.
Mwenyekiti wa chama hicho, Angelique Coetzee, aliliambia shirika la utangazaji la BBC hadi kwa wakati huu visa vilivyogunduliwa nchini humo havijafika katika kiwango kibaya.
Amesema idadi kubwa ya wagonjwa wanalalamikia maumivu ya mwili na uchovu mkali, na kwamba wanaowashuhudia kwa sasa ni vijana zaidi na si watu wazima.Hata hivyo, amesema utafiti kuhusu aina hiyo mpya ya virusi bado upo katika hatua ya mwanzo, na kuongeza pia takwimu za taifa hilo zinaonesha asilimia 24 tu ya raia ndio waliokamilisha chanjo.
Taasisi ya Kudhibiti Magonjwa barani Ulaya, imeonesha wasiwasi mkubwa kuhusu aina hiyo mpya ya virusi kwamba inaweza kupunguza kwa kiwango kikibuwa uwezo wa chanjo zilizopo na kutoa nafasi ya watu kuambukizwa tena.
No comments:
Post a Comment