Mamlaka ya Kikurdi imesema raia watatu wauwawa kwa mripuko - KABATA

This is the special room for news where you need to settle with!


Breaking

Sunday, 28 November 2021

Mamlaka ya Kikurdi imesema raia watatu wauwawa kwa mripuko

 


Wanawake wawili na mtoto mmoja kutoka katika familia moja wameuwawa na wengine watano wamejeruhiwa katika shambilizi lililotokea katika mji wa kaskazini wa Syria wa Minbej.


Baraza la kijeshi la Minbej limesema mripuko ulitokea katika gari la abiria lililokuwa likivuka katika lango la kuingilia mji huo ulio chini ya utawala wa Wakurdi, ambao idadi kubwa ya raia wake wana asili ya Kiarabu.


Kwa upande wake, Shirika la Uangalizi wa Haki za Binaadamu la Syria, lenye maskani yake mjini London, Uingereza, limesema mripuku ulikuwa wa bomu lililotegwa kwenye gari, na kuongoza raia wawili wameuwawa na watano wamejeruhiwa wakiwemo maafisi wa usalama wa Kikurdi.


Wapiganaji wa Kikurdi katika eneo hilo la kaskazini mwa Syria ambao wanalidhibiti eneo kubwa la mashariki na kaskazini mashariki wanaongoza mapambano dhidi ya kundi la Dola la Kiislamu.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here