Migogoro Tigray: Madereva wa teksi waajiriwa kama watoa habari Addis Ababa - KABATA

This is the special room for news where you need to settle with!

Saturday, 20 November 2021

Migogoro Tigray: Madereva wa teksi waajiriwa kama watoa habari Addis Ababa

 


Nchini Ethiopia, mazungumzo yanaendelea kati ya waasi wa kundi la TPLF na serikali ya shirikisho ya Ethiopia. Kusitishwa kwa mapigano kunaweza kuwezekana hivi karibuni, vyanzo kadhaa vya kidiplomasia, ikiwemo Umoja wa Afrika vimebaini. Lakini pamoja na juhudi hizi za amani, uhamasishaji unaendelea.


Serikali imetoa wito kwa wanaume kujiunga na jeshi au makundi ya kujihami ya wanamgambo. Hata madereva wa teksi wanaajiriwa na manispaa ya jiji la Addis Ababa.


Takriban madereva 300 wa teksi wanapokea mafunzo kutoka kwa Manispaa ya jiji la Addis Ababa. “Wananchi wote lazima wawe macho na masikio ya serikali. Lazima kabisa wachangie. Kulingana na Tibebu Bekele, wa ofisi ya Utamaduni na Sanaa ya manispaa ya jiji hilo, huku akiongoeza madereva hao wana mawasiliano ya karibu na mamlaka. "Wanajua wapi pa kwenda na jinsi ya kuripoti. Hata tuliwapa maagizo. Wanaweza kutoa ripoti katika vituo vya polisi au kupitia kituo maalum cha kupiga simu. "


Alemayehu ni dereva kwa miongo miwili. Anashutumu watu wanaoshukiwa kuunga mkono chama cha TPLF huko Tigray. "Tuna Ethiopia moja tu, hakuna kilicho juu yake, lazima tutetee hilo. Kundi la TPLF limetangazwa kama kundi la kigaidi. Kwa hiyo haiwezekani kuishi tukijua kuwa kuna wafuasi wa TPLF miongoni mwetu. "


Mindaw Nigusse anaegesha teksi yake mbele ya uwanja wa ndege wa kimataifa na pia anaangalia harakati za kila mmoja. "Serikali imetangaza nambari ya simu isiyo kuwa na malipo ambayo tunaweza kupiga ili kuwataja wale wanaofanya vitendo vinavyotia hofu na mashaka. "


Kulingana na manispaa ya jiji la Addis Ababa, "karibu watu 200,000 wamejitolea" kujiunga na makundi ya kujihami ya wanamgambo.

No comments:

Post a Comment