Mjumbe wa Marekani kukutana na Taliban mjini Doha - KABATA

This is the special room for news where you need to settle with!


Breaking

Wednesday, 24 November 2021

Mjumbe wa Marekani kukutana na Taliban mjini Doha

 


Mjumbe maalum wa Marekani kwa Afghanistan Tom West atafanya ziara mjini Doha wiki ijayo kwa ajili ya kufanya mkutano na viongozi wa kundi la Taliban. 


Msemaji wa wizara ya mambo ya nje wa Marekani Ned Price amesema mjumbe huyo maalum atajadiliana na Taliban juu ya vita dhidi ya ugaidi, hali ya kiuchumi pamoja na masuala mengine muhimu yanayoihusu Afghanistan. Mapema mwezi huu, West alihudhuria mkutano na wajumbe wa Pakistan, China, Urusi na kujadili juu ya kadhia ya Afghanistan. 


Mjumbe huyo maalum wa Marekani kwa Afghanistan pia alikuwa sehemu ya ujumbe wa Marekani katika mikutano na maafisa wa Taliban mjini Doha mnamo mwezi Oktoba, mazungumzo ya kwanza kabisa kati ya Washington na Taliban baada ya wanajeshi wa Marekani kuondoka Afghanistan mwezi Agosti.


Afghanistan inakabiliwa na uhaba wa fedha wakati viongozi wa Taliban wakiwekewa vikwazo na mataifa ya Magharibi.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here