Mvua yaleta maafa Tabora, yaua watatu - KABATA

This is the special room for news where you need to settle with!


Breaking

Friday, 26 November 2021

Mvua yaleta maafa Tabora, yaua watatu

 


Mvua zilizoanza kunyesha katika baadhi ya maeneo mkoani Tabora zisababisha vifo vya watu watatu akiwamo mtoto wa mwaka mmoja.


Watu hao wamefariki baada ya mvua iliyoambatana na radi kuunguza nyumba waliokuwemo.


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Richard Abwao amesema kuwa tukio hilo limetokea Novemba 25, 2021 katika kitongoji cha Mkuyuni, Kijiji cha Lumbulasiasa kata ya Ugunga Wilaya ya Kaliua.


Amesema wakati mvua inanyesha, radi radi ilipiga na kuiunguza nyumba ambayo walikuwemo.


Amewataja waliofariki kuwa ni John Matelemki (48), Mbisi Maziku (28) na mtoto wa mwaka mmoja, Raphael John.


Kamanda Abwao ametoa wito kwa wananchi kuchukua tahadhari kipindi hiki cha mvua ambazo zimeanza kunyesha katika baadhi ya ya mkoa huo.


"Tunawataka wananchi kuhakikisha Wanaochukua tahadhari wasije kudhurika na mvua hizi zinazonyesha kipindi hiki"amesema

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here