Tetesi za Soka Ulaya Jumanne 30.11.2021: Torres, Pogba, Martial, Brozovic, Phillips - KABATA

This is the special room for news where you need to settle with!

Tuesday, 30 November 2021

Tetesi za Soka Ulaya Jumanne 30.11.2021: Torres, Pogba, Martial, Brozovic, Phillips

 

th

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Barca pia wanavutiwa na mshambuliaji wa Manchester United Mfaransa Anthony Martial, 25. (Marca in Spanish).

Barcelona wana nia ya kumsajili mshambuliaji wa Manchester City na Uhispania Ferran Torres, 21. (Mundo Deportivo, in Spanish)

Viongozi wa Barcelona wamezungumza na wawakilishi wa Torres katika sherehe za Ballon d'Or. (Sport in Spanish)

t

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Kiungo wa kati wa Manchester United na Ufaransa Paul Pogba, 28, hivi majuzi alizungumza na rais wa Paris St-Germain Nasser Al-Khelaifi lakini klabu hiyo ya Ufaransa inasisitiza kuwa haikuwa kitu zaidi ya kukutana tu.(The Athletic)

West Ham wanavutiwa na mlinzi wa kati wa Liverpool Nathaniel Phillips, 24. (Football Insider)

Leeds wanafikiria kumnunua mshambuliaji wa Real Madrid Mariano Diaz, 28, ambaye ana mechi moja katika Jamhuri ya Dominika.(Fichajes.net)

th

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Malang Sarr wa Chelsea, 22, analengwa na Inter Milan. Beki huyo wa Ufaransa amecheza mechi tatu pekee tangu ajiunge nayo mwaka 2020.(Sport Mediaset via Sun)

Newcastle wanampango wa kutumia ''kiasi kikubwa cha fedha'' kumnasa kiungo wa kati wa Inter Milan Marcelo Brozovic,29. (The Athletic, subscription required)

Flamengo wanafikiria kumnunua mlinzi wa kati wa Arsenal na Uhispania Pablo Mari Januari 28.(Football London)

Espirito Santo anataka kurejea haraka kwenye uongozi kufuatia kufukuzwa kwake na Tottenham lakini kuna uwezekano wa klabu ya Ligi ya Premia kuliko kuripotiwa kuhamia Ligue 1.(Le 10 Sport, in French)


No comments:

Post a Comment