Yanga yatamba na ushindi tu kila mechi - KABATA

This is the special room for news where you need to settle with!

Friday, 26 November 2021

Yanga yatamba na ushindi tu kila mechi

 


Kocha wa Yanga, Mtunisia Mohammed Nasreddine Nabi amesema mchezo dhidi ya Mbeya Kwanza wa Ligi kuu NBC Tanzania utakaichezwa Novemba 30, 2021 utakuwa mchezo mgumu lakini anahitaji ushindi kila mechi.


Nabi amesema: "Itakuwa mechi yenye mvuto, tunakutana na timu mpya kwenye Ligi, lakini katika soka hakuna udogo tumejianda kuendelea kuwapa furaha mashabiki wetu. Tunahitaji ushindi katika kila mechi"


Mpaka sasa Yanga ni kinara wa msimamo wa Ligi kuu ya NBC Tanzania akiwa na alama 16 baada ya kushindi michezo yake 5 mfululizo na kupata sare moja dhidi ya Namungo juma lililopita.


Kwa upande wa Mbeya Kwanza, ipo nafasi ya 8 ikiwa na alama 7 baada ya kucheza michezo 6, ikipata ushindi kwenye mchezo 1, sare 4 na kipigo 1. 

No comments:

Post a Comment