th

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Newcastle United wanazidi kuwa na uhakika wa kumsajili beki wa Uingereza Kieran Trippier, 31, kutoka Atletico Madrid mwezi ujao. (Football Insider)

Kocha wa Chelsea Thomas Tuchel anasema atawasiliana na Pierre-Emerick Aubameyang baada ya mshambuliaji huyo wa Gabon, 32, kuvuliwa unahodha wa Arsenal.

(Mirror)

Barcelona wanajiandaa kumnunua mshambuliaji wa Borussia Dortmund na Norway Erling Braut Haaland, 21.(Sport)

th

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Manchester City pia wanavutiwa na Haaland lakini wanaweza kutokuwa tayari kutumia pesa za kutosha kumpata.(Manchester Evening News)

Arsenal, Tottenham na Manchester United wako tayari kumtaka Dusan Vlahovic baada ya habari kwamba mshambuliaji huyo wa Serbia mwenye umri wa miaka 21 alikataa "mkataba wa juu zaidi katika historia ya Fiorentina".(Talksport)

th

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Mlinzi wa Chelsea na Ujerumani Antonio Rudiger, 28, ambaye amebakiza miezi sita katika mkataba wake, amethibitisha kuwa anafikiria kuondoka katika klabu hiyo kabla ya Thomas Tuchel kuteuliwa kuwa meneja mwezi Januari.(Sky Sports via Mirror)

TH

CHANZO CHA PICHA,PA MEDIA

Kocha wa Liverpool Jurgen Klopp anasema mlinzi wa Uingereza Joe Gomez, 24, hataondoka na kujiunga na Steven Gerrard huko Aston Villa katika dirisha la uhamisho la Januari.(Express)

Kiungo wa kati wa RB Leipzig Amadou Haidara, 23, amechochea uvumi unaomhusisha na Manchester United baada ya kumsifu kocha wa muda wa klabu hiyo Ralf Rangnick.(Bild,via Express)

Mshambuliaji wa Inter Milan Alexis Sanchez, 32, anaweza kurejea Barcelona kwa mkopo, huku mshambuliaji Luuk de Jong, 31, ambaye kwa sasa yuko kwa mkopo Barca kutoka Sevilla, akihamia Inter.(Sport)

TH

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Mlinzi Nat Phillips, 24, amekiri kwamba yuko tayari kuondoka Liverpool mwezi Januari kutafuta soka la kawaida.(Sky Sports,via Liverpool Echo)

Middlesbrough wako kwenye mazungumzo ya kusajili washambuliaji wawili kwa mkopo mwezi ujao.(Football Insider)

West Ham ni miongoni mwa vilabu vya Ulaya vinavyotaka kumsajili mlinzi wa Argentina anayechezea Feyenoord Marcos Senesi, 24. (90min)