Sevilla wamejiunga na Barcelona katika kinyang'anyiro cha usajili wa mshambuliaji wa Uruguay Edinson Cavani, 34, Manchester United. (Mundo Deportivo - in Spanish)
AC Milan wanamatumaini ya kumsajili winga wa Chelsea na Morocco Hakim Ziyech, 28. (Calciomercato - in Italian)
Liverpool wanapania kumnunua kiungo wa kati wa Real Madrid na Ufaransa Eduardo Camavinga, 19. (El Nacional - in French)
Newcastle United wamewasiliana na wawakilishi wa mshambuliaji wa Barcelona na Ufaransa Ousmane Dembele, 24, ijapokuwa klabu hiyo ya Uhispania inajaribu kurefusha mkataba wake. (Fabrizio Romano)
Tottenham wanatathini uwezekano wa kumnunua beki wa Juventus na Uholanzi Matthijs de Ligt, 22. (4-4-2 via Sun)
Kiongo wa kimataifa wa Uingereza na Arsenal wachini ya miaka 21 Eddie Nketiah, 22, anataka kuondoka kwa ajili ya kutaka kucheza katika kikosi cha kwanza licha ya The Gunners kutaka kuongeza mkataba wake utakaokamilika msimu ujao wa joto. (Mail)
Juventus wanataka kumsajili mshambuliaji wa Manchester United Mfaransa Anthony Martial, 26, na mshambuliaji wa Arsenal na Gabon Pierre-Emerick Aubameyang, 32. (Gazzetta dello Sport, usajili unahitajika)
Klabu hiyo ya Italia pia ina nia ya kutaka kumnunua mshambuliaji wa Fulham mwenye umri wa miaka 27 kutoka Serbia Aleksandar Mitrovic. (90 Mins)
Ralf Rangnick anajiandaa kuwasiliana na klabu yake ya zamani ya RB Leipzig kumnunua kiungo wa kati wa Mali Amadou Haidara, 23, huku akitafuta mbadala wa Nemanja Matic, 33, raia wa Serbia, Manchester United. (Mirror)
No comments:
Post a Comment