Tetesi za soka Ulaya Jumanne tarehe 07.12.2021: Azpilicueta, Dembele, De Jong, Mee, Messi, Ibrahimovic - KABATA

This is the special room for news where you need to settle with!


Breaking

Tuesday, 7 December 2021

Tetesi za soka Ulaya Jumanne tarehe 07.12.2021: Azpilicueta, Dembele, De Jong, Mee, Messi, Ibrahimovic

 

Minzi wa Chelsea Mhispania Cesar Azpilicueta

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,

Minzi wa Chelsea Mhispania Cesar Azpilicueta

Mlinzi wa Chelsea Mhispania Cesar Azpilicueta, 32, anafanya mazungumzo na Barcelona juu ya uhamisho msimu huu. (El Nacional, via Daily Mail)

Meneja wa Newcastle Eddie Howe amemuorodhesha mshambuliaji wa Stoke mwenye umri wa miaka 21- Tyrese Campbell kama mchezaji wa kwanza wa enzi ya Saudi katika St James' Park. (Sun)

Ousmane Dembele

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,

Ousmane Dembele

Manchester United wamejiunga na klabu ya Primia Ligi inayohangaika Newcastle United katika kumsaka winga wa Barcelona Ousmane Dembele, huku mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 24 akiwa amefanya uamuzi juu ya hali yake ya baadaye. (Mundo Deportivo, via Express)

Newcastle wanajianda kuongeza mishahara mara dufu kwa Mlinzi Muingereza anayechezea klabu ya Burnley Ben Mee, 32, na James Tarkowski mwenye umri wa miaka 29-kujaribu kuwashawishi waondoke Newcastle. (Mirror)

Meneja mpya wa Manchester United Ralf Rangnic

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,

Meneja mpya wa Manchester United Ralf Rangnic

Meneja mpya wa Manchester United Ralf Rangnick anafuatilia kwa karibu kwa lengo la uhamisho wa kiungo wa kati wa Uholanzi Frenkie de Jong mwenye umri wa miaka , 24, ambaye kwa sasa yuko Barcelona huku akianza mchakato wa kujenga upya kikosi chake katika Old Trafford. (El Nacional, via Daily Star)

Hatua ya Chelsea ya kumchukua mlinzi wa Fenerbahce mwenye umri wa miaka 23 Attila Szalai ni "mpango uliokamilika", kulingana na meneja wake Mhangary Marco Rossi. (Mirror)

Winga Mnorway na ambaye analengwa na Arsenal Mohamed Elyounoussi

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,

Winga Mnorway Mohamed Elyounoussi

Winga Mnorway na ambaye analengwa na Arsenal Mohamed Elyounoussi, 27, amesisitiza kuwa yeye na familia yake wanafurahia maisha katika klabu ya Southampton. (Sun)

Manchester United wanaangalia uwezekano wa kumkodisha kiungo wa zamani wa kati , ambaye ni mchezaji wa kimataifa wa Marekani kocha aliyeongoza mara mbili katika Ligi kuu ya soka Chris Armas, 49, kama sehemu ya wafanyakazi wa Ralf Rangnick. (ESPN)

Mshambuliaji wa AC Milan Msweden Zlatan Ibrahimovic

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,

Mshambuliaji wa AC Milan Msweden Zlatan Ibrahimovic

Mshambuliaji wa AC Milan Msweden Zlatan Ibrahimovic, 40, ameelezea matamanio yake ya kuendelea kubakia katika klabu hiyo ya Serie A club hadi mwisho wa kazi yake ya soka (Star)

Mlinzi wa Ureno Diogo Dalot, 22, amekuwa akitoa jumbe za kusisitiza kuwa yuko tayari ku "toa kila kitu" katika Manchester United katika kile kinachoonekana kuwa ni pigo kwa klabu nyingine zinazomtaka. (Daily Mail)

Lionel Messi ameanza kuhoji iwapo Mauricio Pochettino

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,

Lionel Messi ameanza kuhoji iwapo Mauricio Pochettino

Lionel Messi ameanza kuhoji iwapo Mauricio Pochettino yuko tayari kuchukua kazi kama meneja wa Paris St-Germain baada ya mshambuliaji huyo Muargentina mwenye umri wa miaka 34 34-kuelezea hofu zake kuhusu mbiny na uwezo wa kudhibiti kudhibiti wachezaji ndani ya chumba cha kuvaa. (L'Equipe, via Mirror)

Pierre-Emerick Aubameyang

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,

Pierre-Emerick Aubameyang

Arsenal wanaonekana wako tayari na kuondoka kwa mshambuliaji wa kimataifa wa kikosi cha vijana wadogo cha England mwenye umri 20 Folarin Balogun -mwezi Januari - licha ya kukabiliwa na uwezekano wa kumkosa mshambuliaji Kutoka Gabon mwenye umri wa miaka 32 Pierre-Emerick Aubameyang katika kipindi cha hadi mwezi mmoja wakati wa michuano ya mwezi mmoja Kombe la mataifa ya Afrika . (Express)

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here