Wakenya wapata faraja mashambani baada ya corona kuwatimua mjini - KABATA

This is the special room for news where you need to settle with!

Thursday, 16 December 2021

Wakenya wapata faraja mashambani baada ya corona kuwatimua mjini

 


Geoffrey Barasa sasa anafanya shughuli za kilimo magharibi mwa Kenya baada ya kupoteza kazi mara mbili

CHANZO CHA PICHA,WORLD NEIGHBOURS

Maelezo ya picha,

Geoffrey Barasa sasa anafanya shughuli za kilimo magharibi mwa Kenya baada ya kupoteza kazi mara mbili

Kama janga la Corona halikuwa limetokea, kuna uwezekano Jack Onyango angekuwa bado anaishi peke yake, akifanya kazi katika mji mkuu wa Kenya na kutuma pesa kwa mke wake na watoto wanaoishi mbali kijijini.

Sawa na Wakenya wengi, alihamia Nairobi akiwa kijana, akiamini kwamba huko ndiko kunakopatikana fursa za kiuchumi.

Lakini maisha katika mji mkuu hayakuwa rahisi. Bw. Onyango aliweza tu kusafiri nyumbani kujumuika na familia yake mjini Kisumu, magharibi mwa Kenya mara moja kwa mwaka.

Alisafiri msimu wa Krismasi kwa kulipa nauli ya shilingi 2,000 za Kenya sawa na ($18; £13) - na pia alitarajiwa kununua walau sukari akifika nyumbani awe na kitu cha kupokelewa.

Wakati janga la Corona lilipotokea mwaka 2020, mamlaka ziliweka masharti makali kama vile kudhibiti usafiri na mengine mengi, Bw Onyango alijipata hana ajira.

Wakati serikali katika sehemu zingine za ulimwengu zililipa mishahara nusu kwa wale waliopoteza kazi wakati wa janga hili, nchini Kenya hakukuwa na msaada kama huo.

Jack Onyango aliweza kutembelea familia yake katika kijiji cha Nyakach mara moja tu kwa mwaka

CHANZO CHA PICHA,JACK ONYANGO

Maelezo ya picha,

Jack Onyango aliweza kutembelea familia yake katika kijiji cha Nyakach mara moja tu kwa mwaka

"Hakukuwa na mahali pa kupata pesa za kulipa karo na kulisha familia yangu changa," asema.

Kwa kuwa hakuwa na uwezo wa kuishi jijini, aliamua kurejea kijijini kwao Julai mwaka huo.

"Nilikuwa na wasiwasi lakini nilipiga moyo konde," Bw. Onyango anasema. "Nyumbani hakuwa na gharama ya kulipa kodi, bili ya umeme na maji ukilinganisha na jijini Nairobi ambako kila kitu kinagharimu pesa."

Alianza kulima tomato na mboga za kienyeji katika shamba la hekari 1.5 ambalo wakati mmoja lilikuwa likimilikiwa na babu yake.

Aliuza mazao yake kwa majirani na wafanyabiashara, ambao walipeleka sokoni kuuzia watu wengine.

"Pesa ninazopata kutokana na kile ninachofanya sasa ni nyingi zaidi ikilinganishwa na nilizokuwa nikipata kufanya kazi Nairobi.

"Binti yangu mkubwa ana umri wa miaka 16. Nilikuwa nawaona mara moja kwa mwaka. Kwa kweli, corona imekuwa baraka kwangu."

Maisha ya vijijini yamekuwa faraja

World Neighbors, Shirika la kimataifa la maendeleo linasema alichofanya Onyango ni sehemu ya mwelekeo wa uhamaji usiokuwa wa kawaida, uloisababishwa na janga la corona

1px transparent line

"Covid-19 ilimpata kila mtu ghafla," anasema Chris Macoloo, Mkurugenzi wa Afrika wa shirika hilo.

"Baadhi ya watu walipoteza ajira, kwa sababu wanaishi kwa vibarua vya kila siku kwa mwezi, hawakuwa na uwezo wa kijilisha, kulipa kodi ya nyumba au kutuma pesa za kusaidia familia zao nyumbani. Kutokana na hilo wengi wao walihamia maeneo ya vijijini."

Anasema maisha vijijini yaliwapa faraja watu wengi.

"Barani Afrika sisi ni watoto wa dunia mbili. Tuna mguu mmoja mjini na mwingine mashambani. Ilisaidia kwa sababu tusingekuwa na hayo, wangekuwa kwenye matatizo makubwa."

Takriban ajira 750,000 zilipotea kote nchini Kenya mwaka wa 2020, kulingana na Ofisi ya Kitaifa ya Takwimu ya Kenya.

Ripoti ya hivi karibuni ya shirika hilo ilisema sekta mbalimbali za uchumi zimeathiriwa vibaya na hatua za kudhibiti Covid, na jumla ya ajira, ukiondoa shughuli ndogo za kilimo na ufugaji, zilizopunguzwa kwa asilimia 4.1 hadi milioni 17.4.

Ukulima mdogo unasaidia jamii nyingi kukabiliana na janga hili

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,

Ukulima mdogo unasaidia jamii nyingi kukabiliana na janga hili

Mwanzoni masharti ya kudhibiti virusi vya corona yalipowekwa, serikali ya Kenya ilipiga marufuku usafiri baina ya miji mikuu, na kuibua wasiwasi kuhusu usalama wa chakula wa kikanda katika maeneo ambayo hayazalishi mazao mengi ya ndani.

Matokeo yake, wengi wa wahamiaji wa ndani ambao walirudi nyumbani vijijini waligeukia kulima mboga wenyewe.

Jambo la fahari

Geoffrey Barasa ni Mkenya mwingine aliyeacha maisha ya mjini. Mtu huyo mwenye umri wa miaka 46 aliwahi kushikilia kazi

Nguruwe

CHANZO CHA PICHA,GEOFFREY BARASA

Maelezo ya picha,

Geoffrey Barasa anafanya kilimo cha ufugaji

Aliajiriwa kama mfanyakazi wa kibarua katika eneo la viwanda la jiji na pia alifanya biashara ndogo ya kununua vipande vya kuku sokoni na kuziuza kwa faida katika duka lake la ndani.

Alihamia mjini akiwa kijana baada ya kuhitimu chuo kikuu, akisema "ilikuwa [jambo la] fahari kufanya kazi mjini wakati huo".

Bw. Barasa alioa na kuishi mjini Nairobi na mke wake na watoto wanne,.

Lakini mara baada ya ugonjwa wa corona kuripotiwa nchini Kenya, kila kitu kiliharibika. Alipoteza kazi yake ya kawaida na akalazimika kufunga biashara yake ya kuku.

"Wakati huo watu walikuwa hawatangamani , kwa hivyo sikuwa na wateja wa kununua bidhaa zangu. Nililazimika kufunga biashara yangu na kurudi vijijini," anasema Bw. Barasa.

"Wakati huo nilikabiliwa na hali ngumu sana."

Mnamo September 2020, aliamua kupeleka familia yake kijijini kwao katika jimbo la Busia magharibi mwa Kenya, sio mbali sana na ukingo wa Ziwa Victoria.

Alianza kilimo cha malenge, mtama, tomato na sukuma wiki - na sasa anauza bidhaa zake katika soko la nyumbani. Leo hii anafuga nguruwe na kuku pia.

"Mwanzoni nilikuwa na wasiwasi maisha yatakuwaje vijijini, lakini sasa nimezoea. Naishi vizuri kuliko wakati nilipokwa Nairobi. Nafurahia maisha ya mashambani."

Bw Barasa anawasihi wengine waliorejea nyumbani wakati wa janga hili kufanya hatua ya kudumu: "Siwezi kuwashauri warudi mjini."

No comments:

Post a Comment