Barcelona yamtaka Dembele kuondoka katika klabu hiyo mara moja - KABATA

This is the special room for news where you need to settle with!

Friday, 21 January 2022

Barcelona yamtaka Dembele kuondoka katika klabu hiyo mara moja


Barcelona wamemtaka wing awa timu hiyo Ousmane Dembele kuondoka kwa lazima mwezi huu kwasababu hayupo katika mradi wa timu hiyo.


Dembele atakuwa mchezaji huru mwisho wa msimu hu una amedaiwa kukataa ofa ya mkataba mpya


Alijiunga na Barcelona kutoka Borrusia Dortmund mwaka 2017 katika mkataba uliokuwa na thamani ya £135.5m lakini atalazimika kuondoka bure mkataba wake utakapokamilika .


"Inaonekana wazi kwamba mchezaji huyo hataki kusalia katika klabu ya Barca’’ , alisema mkurugenzi wa soka Mateu Alemany.


Mkufunzi wa Barcelona Xavi tayari amemuonya Dembele kwamba ni sharti aweke kandarasi ya mkataba mpya la sivyo aondoke.


Alemany alisema kwamba klabu hiyo inamuunga mkono Xavi na inakubali kwamba , hatua hiyo ndio mwafaka , huku mazungumzo ya kandarasi ya muda mrefu yakikwama.


"Tukiwa na Ousmane Pamoja na ajenti wake , tulianza mazyngymzo ya kandarasi mpya mnamo mwezi Julai hivyobasi mazungumzo hayo yamechukua miezi sita’’,Alemany said.


‘’Tumezungumza , tumezungumza , tumezungumza . Barca imewasilisha maombi tofauti. Tumejaribu kumtafuta njia kuendelea nasi lakini maombi hayo yamekataliwa na ajenti wake’’


‘’Kutokana na hilo yeye na na maajenti wake wametakiwa ni sharti aondoke mara moja kwasababu tunataka wachezaji amabo wako tayari kusalia katika klabu hiyo na sasa inatumai kwamba uhamisho qutafanyika kabla ya Januari 31’’

No comments:

Post a Comment