Ethiopia yamuachia huru kiongozi wa upinzani na wengine - KABATA

This is the special room for news where you need to settle with!

Saturday, 8 January 2022

Ethiopia yamuachia huru kiongozi wa upinzani na wengine


Chama cha upinzani nchini Ethiopia cha Balderas kwa demokrasia halisi chake Eskinder Nega, kimesema kiongozi huyo ameachiwa huru kutoka gerezani baada ya kusota jela kwa mwaka mmoja na nusu.


Kituo cha televisheni kinachomilikiwa na serikali ya Ethiopia kimetangaza kuwa kiongozi mwengine wa upinzani kutoka jamii ya Oromo, Bekele Garba, pamoja na Jawar Mohammed ambaye ni mwanasiasa na mmiliki wa chombo cha habari pia wameachiwa huru.


Eskinder aliyekianzisha chama cha Balderas alikamatwa mwaka 2020 kufuatia machafuko yaliyozuka kutokana na kuuawa kwa mwanamuziki na pia mwanaharakati Hachalu Hundessa.Eskinder alishtakiwa mwezi Septemba mwaka 2020, kwa madai ya ugaidi katika mahakama kuu nchini Ethiopia. 


Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amekaribisha hatua ya kuachiwa huru kwa Eskinder. Amesema anatumai juhudi zakuwezesha misaada ya kiutu kufikia maeneo ambayo yameathiriwa kutokana na vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini humo zitaimarishwa.


Vikosi vya serikali ya Ethiopia vimekuwa vikipambana na waasi katika jimbo la Tigray kwa muda wa mwaka mmoja sasa.Katika wiki za hivi karibuni, Waziri Mkuu wa nchi hiyo Abiy Ahmed, alisema nchi

No comments:

Post a Comment