Mwanaume akatwa kichwa Msumbiji katika shambulio la imani za kishirikina - KABATA

This is the special room for news where you need to settle with!


Breaking

Monday, 17 January 2022

Mwanaume akatwa kichwa Msumbiji katika shambulio la imani za kishirikina




Polisi nchini Msumbiji wanasema kichwa cha mwanaume mwenye upara kimekatwa na kuondolewa na wahalifu waliotaka kukiuza kwa mteja wao nchini Mali.

Wakati mteja wao alipotoweka, walikiacha kichwa hicho katika mji wa kati wa Muandiwa.

Baadhi ya watu wa Msumbiji wanaamini kuwa kichwa cha mwanaume mwenye upara huwa kina dhahabu ndani yake.

Ripoti ya kwanza kuhusu kuuawa kwa wanaume wenye upara kwa ajili ya kuchukua vichwa vyao ziliripotiwa mwa 2017.

Biashara ya viungo vya binadamu ni jambo la kawaida katika nchi za Msumbiji, Malawi na Tanzania ambako vinaaminiwa kuleta utajiri na bahati katika mapenzi.

Sehemu za miili ya watu wenye ulemavu wa ngozi (ualbino) huuzwa kwa bei ghali.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here