Rafael Benitez: 'Sikujua uzito wa jukumu nililopewa Everton' - KABATA

This is the special room for news where you need to settle with!

Monday, 17 January 2022

Rafael Benitez: 'Sikujua uzito wa jukumu nililopewa Everton'


Everton inatarajiwa kumuajiri Dancun Fergusonna Leighton Baines kuwa kaimu wakufunzibaada ya kumfuta kazi Rafael Benitez.


Hapo jana muda mfupi baada ya kupigwa kalamu Benitez alisema kwamba hakujua uzito wa jukumu alilopewa katika klabu hiyo baada ya kufutwa chini ya miezi saba ya kuhudumu.


The Toffees waliamuajiri kocha huyo wa zamani wa Liverpoolkuwa mrithi wa Carlo Ancelotti.


Everton imeshinda mechi moja kati ya 13 za ligi ya Premiana wako katika nafasi ya 16 katika jedwali la ligi , alama sita juu ya eneo la kushushwa daraja.


‘’Tulijua haitakuwa rahisi’’, Benitez alisema alipokuwa akiondoka.


‘’Ilikuwa changamoto kubwa, kihisia na kimichezo. Upendo wangu wa mji huu , na watu wakeulinifanya kukubali changamoto hii, lakini ni wakati unapokuwa ndani ndiposa unapogundua uzito wa jukumu ulilopewa’’.


‘’Kuanzia siku ya kwanza , wafanyakazi wangu na mimi mwenyewe tulifanya kazi kama kawaida, kwa kujizatiti . Hatukuweza kupata matokoe mazuri lakini tulivutia nyoyo za wengi’’.

No comments:

Post a Comment