Simba yapigwa na kitu kizito Mbeya - KABATA

This is the special room for news where you need to settle with!


Breaking

Monday, 17 January 2022

Simba yapigwa na kitu kizito Mbeya


Mbeya City wameinyoosha Simba kwa bao 1-0 lililopachikwa na Paul Nonga mapema kipindi cha kwanza katika dimba la Sokoine Jijini Mbeya.

Haikuwa rahisi kwa Simba kuweza kumtungua kipa namba moja wa Mbeya City, Deogratius Munish ambaye alikuwa kwenye ubora wake mwanzo mwisho.

Huu unakuwa ni mchezo wa kwanza kwa Simba kupoteza ndani ya Ligi Kuu Bara kwa msimu wa 2021/22.

Aishi Manula jitihada zake za kuokoa michomo hazikuzaa matunda kwa kuwa aliokota mpira mmoja nyavuni na kuifanya timu ya Simba kuyeyusha pointi tatu mazima.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here