Thomas Muller

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Mshambuliaji wa Bayern Munich na Ujerumani Thomas Muller amezivutia Newcastle United na Everton, huku mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 32 akikaribia mwaka wa mwisho wa kandarasi yake na timu hiyo ya Bundesliga.(Sportbild - via Star)

Barcelona wanafanyia kazi mpango wa kuchangisha €100m (£83.5m) kufadhili usajili wa mshambuliaji wa Borussia Dortmund na Norway Erling Haaland mwenye umri wa miaka 21 msimu huu.(Goal)

Erling Haaland

CHANZO CHA PICHA,REUTERS

Brighton wamekataa ofa kutoka kwa Newcastle kwa ajili ya mlinzi wa Uingereza Dan Burn, 29. (Athletic - subscription required)

Kiungo wa kati wa Lyon Bruno Guimaraes ameiambia klabu hiyo kuwa anataka kuhamia Newcastle, ambayo imewasilisha ofa mezani kwa Mbrazili huyo mwenye umri wa miaka 24. (L'Equipe)

Bruno Guimaraes

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Frank Lampard sasa ndiye anayeongoza kuwania nafasi ya kocha wa Everton. (Independent)

Southampton wanatayarisha dau la rekodi la klabu la £25m kumpa Armando Broja kandarasi ya kudumu baada ya mchezaji huyo wa kimataifa wa Albania mwenye umri wa miaka 20 kujiunga na klabu hiyo kutoka Chelsea kwa mkopo wa msimu mmoja mwanzoni mwa msimu. (Fabrizio Romano)

Armando Broja

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Newcastle wameanza tena mazungumzo ya kumsajili mlinzi wa Uholanzi Mitchel Bakker kutoka Bayer Leverkusen, huku klabu hiyo ya Bundesliga ikiwa na nia ya kumuuza mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21 kwa Magpies kwenye dirisha la Januari. (90 min)

Lakini Magpies wanaonekana kuchanganyikiwa katika harakati zao za kumnunua Jesse Lingard kwa mkopo kwani Manchester United wanadai ada kubwa mno kwa mchezaji wa kimataifa wa Uingereza mwenye umri wa miaka 29. (Mail)

Jesse Lingard

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Tottenham wamekubali kumtoa kwa mkopo kiungo wa kati wa Ufaransa Tanguy Ndombele, 25, kwenda Valencia. (Telefoot)

Winga wa Wolves Muhispania - na anayelengwa na Tottenham - Adama Traore, 26, pia sasa anatazamwa kama chaguo kwa Barcelona ikiwa wanaweza kupata dili la kumhamisha mshambuliaji wa Kifaransa Ousmane Dembele, 24, nje ya klabu hiyo. (ESPN)

Liverpool wamefanya mawasiliano na mshambuliaji wa Juventus na Argentina Paulo Dybala, huku mkataba wa sasa wa mchezaji huyo wa miaka 28 ukikamilika msimu wa joto. (TuttoMercato - via Sun)

Paulo Dybala

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Mlinzi wa Liverpool Muingereza Nat Phillips, 24, anawindwa na Newcastle, West Ham na Watford. (Independent)

Matumaini ya Arsenal kumsajili kiungo wa kati wa Brazil Arthur Melo, 25, kwa mkopo hadi mwisho wa msimu kutoka Juventus yako mashakani. Miamba hao wa Serie A wanatafuta makubaliano ya miezi 18. (Athletic - subscription required)

Arsenal wanatarajiwa kuimarisha harakati zao za kumnunua kiungo wa kati wa Aston Villa Mbrazil Douglas Luiz, 23, kabla ya dirisha la uhamisho kukamilika. (Birmingham Mail)

Douglas Luiz

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Leicester wanajaribu kumsajili mshambuliaji wa Angers mwenye umri wa miaka 18 Mohamed Ali-Cho, huku Mfaransa huyo pia akihusishwa na Tottenham. (Footmercato - via Leicester Mercury)

West Ham na Crystal Palace wanatazamia kutaka kumnunua mshambuliaji wa Senegal na Marseille Bamba Dieng, 21, huku timu hiyo ya Ufaransa ikiwa tayari kumwachia mwezi huu kwa pauni milioni 8. (RMC Sport - via Mail)

Manchester City wanajiandaa kumsajili winga wa Hungary Zalan Vancsa mwenye umri wa miaka 17 kutoka MTK Budapest. (Telegraph)

AC Milan wamewasilisha ofa kwa mshambuliaji wa Arsenal Pierre-Emerick Aubameyang lakini mchezaji huyo wa kimataifa wa Gabon, 32, amedai zaidi ya mara mbili ya anacholipwa Zlatan Ibrahimovic katika klabu hiyo ya Italia. (Star)

Pierre-Emerick Aubameyang

Brighton wameona ombi lao la kumnunua mshambuliaji wa Uhispania Abel Ruiz, 21, limekataliwa na Braga. (dakika 90)

Mlinzi Mfaransa William Saliba, 20, anataka kurejea Arsenal kutoka Marseille alikokuwa akicheza kwa mkopo , licha ya tetesi zinazosema kuwa anaweza kujiunga na klabu hiyo ya Ligue 1 kwa mkataba wa kudumu. (football.london)

Tottenham wanaweza kumtumia kiungo wa kati wa Argentina Giovani Lo Celso kama sehemu ya makubaliano ya kumsajili mlinzi wa kati wa Brazil na anayelengwa na Newcastle Diego Carlos, 28, kutoka Sevilla. (Sun)