United wametoa ofa kwa kiungo wa kati Mfaransa Paul Pogba, 28,ya mkataba wenye thamani ya pauni 500,000 kwa wiki ili aendelee kubakia katika klabu hiyo . (Sun)
Pogba, hatahivyo, amekana kupewa ofa ya mkataba mpya . (Mail)
Manchester United wanawinda saini ya kiungo wa kati wa Lazio na Serbia Sergej Milinkovic-Savic, 26. (Calciomercato - in Italian)
Mashetani wekundu wamemaliza nia yao ya kusaini mktaba na mshambuliaji wa Norway na Borussia Dortmund Erling Haaland. (Mirror)
Mmiliki wa zamani wa Newcastle Mike Ashley anafikiria kuchukua dau la kuinunua klabu ya Derby County(Telegraph)
Liverpool wako tayari kumpa kiungo wa kati wa Barcelona na Uhispania Gavi, 17, karibu pauni 80,000 kwa wiki ili kunasa saini yake. (El Nacional - via Mail)
Lakini Manchester City pia wana nia ya kumsajili Gavi, ambaye ana kipengee cha kuachiliwa kwa pauni milioni 42 katika mkataba wake(El Nacional, via Mail)
Liverpool wanajiandaa kutoa ofa ya mkataba kwa kiungo wa kati wa Barcelona na Uhispania Gavi, 17, wa malipo ya karibu pauni 80,000 kwa wiki ili kupata sahihi yake. (El Nacional - via Mail)
Lakini Manchester City pia wana nia ya kusaini mkataba na Gavi, ambaye ana kipengele cha kumuachilia cha pauni milioni 42 katika mkataba wake. (El Nacional, via Mail)
Everton wamepewa ofa ya mshambuliaji wa zamani wa Arsenal na Manchester United wa Inter Milan Alexis Sanchez, 33, kwa uhamisho wa bila malipo. (Sun)
Newcastle wameongeza dau lao kwa mlinzi wa Lille Sven Botman, 21. (Newcastle Chronicle)
Aston Villa wanavutiwa na kiungo wa kati wa Brighton wa Mali, Yves Bissouma, 25(Sky Sports)
Mkufunzi wa Paris St-Germain Mauricio Pochettino yuko tayari kupokea ofa yoyote ya kuwa kocha wa Manchester United. (Sun)
West Ham itakataa ofa yoyote ambayo Newcastle itampa mlinzi wa Ufaransa Issa Diop, 24 (Football London)
Liverpool wamekataa dau la pauni milioni 7 kutoka kwa Watford kwa ajili ya mlinzi wa Uingereza Nathaniel Phillips, 24. (Football Insider)
Meneja Brendan Rodgers amefichua kuwa ana hamu ya kusajili beki wa kati kwa mkopo Leicester. (Leicester Mercury)
Sevilla hawako tayari kumruhusu mlinzi wa Brazil Diego Carlos, 28, ajiunge na Newcastle kwa chochote isipokuwa ada kubwa. (Daily Star)
The Reds pia hawako tayari kumruhusu mshambuliaji wa Ubelgiji Divock Origi, 26, kuondoka kwa bei iliyopunguzwa Januari. (Liverpool Echo)
Kiungo wa kati wa Arsenal na Uingereza Ainsley Maitland-Niles, 24, amewasili Italia kabla ya kuhamia kwa mkopo katika klabu ya Serie A ya AS Roma. (football.london
Kiungo wa kati wa AC Milan Franck Kessie yuko kwenye mazungumzo juu ya kuhamia Real Madrid licha ya Liverpool na Tottenham kuonyesha nia ya kumnunua mchezaji huyo wa kimataifa wa Ivory Coast mwenye umri wa miaka 25. (El Nacional - in Italian)
Chelsea wanatafuta njia za kuziba upande wa kushoto wa safu ya ulinzi wakati Ben Chilwell hayupo, pamoja na kuzungumza na Lyon kuhusu kumnunua beki wa kushoto wa Italia Emerson Palmieri, 27, ambaye yuko kwa mkopo katika klabu hiyo ya Ufaransa. (Evening Standard)
Barcelona ndio klabu ya hivi punde zaidi kufuatilia hali ya Antonio Rudiger katika klabu ya Chelsea huku beki huyo wa kimataifa wa Ujerumani mwenye umri wa miaka 28 akimaliza mkataba wake mwishoni mwa msimu huu. (Sky Sports)
Arsenal wametoa ofa ya mchezaji zaidi ya pesa kumnunua mshambuliaji wa Fiorentina na Serbia Dusan Vlahovic, 21.(Ben Jacobs - CBS)
Mshambulizi wa Argentina Lionel Messi, 34, anaweza kulazimisha kuondoka kwake Paris St-Germain baada ya msimu mmoja tu ikiwa klabu hiyo itashindwa kushinda Ligi ya Mabingwa, kulingana na kiungo wa kati wa zamani wa Barcelona na timu ya taifa ya Uhispania Lobo Carrasco. (El Chiringuito TV, via Mirror)
Manchester United hawana mpango wa kufanya usajili wowote mwezi huu lakini watamtafuta kiungo wa kati msimu wa joto, huku mchezaji wa kimataifa wa Uingereza mwenye umri wa miaka 22 Declan Rice akipigiwa upato kujiunga nao. (Mchezo)
No comments:
Post a Comment