Thomas Partey
Juventus inamnyatia kiungo wa kati wa Arsenal na raia wa Ghana Thomas Partey, 28, kushirikishwa katika mkataba wowote wa klabu hiyo ya serie A wa kiungo wa kati wa Brazil Arthur Melo, 25. (Sky Sports Italy, via Mail)
Newcastle United inafikiria kuwasilisha ombi la kutaka kumsajili kipa wa klabu ya PSG Keylor Navas lakini klabu hiyo ya Ligue 1 inataka kumdhibiti kipa huyo mwenye umri wa miaka 35 raia wa Costa Rica na kwamba hawako tayari aondoke. (RMC Sport via Mail)
Winga wa Ufaransa na Barcelona Ousmane Dembele anatarajiwa kuondoka katika klabu hiyo ili kujiunga na Manchester United au Juventus huku Chelsea na Bayern Munich wakiwa wametupwa nje katika harakati za kumsaini mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24. (Sport - in Spanish)
Kiungo wa kati wa Manchester United raia wa Uholanzi Donny van de Beek, 24, amekataa ombi la yeye kujiunga na klabu ya Newcastle kwa mkopo kutokana na nafasi ilio klabu hiyo katika jedwali la ligi ya premia . (Telegraph - subscription required)
Newcastle inapiga hatua katika majaribio yao ya kutaka kumsajili beki wa Sevilla na Brazil mwenye umri wa miaka 28 Diego Carlos. (Express)
Hatahivyo , the Magpies wameshindwa katika jaribio lao la kumsajili beki wa kati raia wa Uholanzi Sven Botman, 22, kutoka Lille. (90min)
Chelsea ina hamu ya kumsajili beki wa PSG raia wa Ufaransa Layvin Kurzawa, 29, kwa mkopo lakini mazungumzo hayajaanza kati yao. (Fabrizio Romano on Twitter)
Southampton ipo katika mazungumzo na Chelsea kuhusu uhamisho wa kudumu wa raia wa Alabania ambaye anahudumu katika klabu hiyo kwa mkopo , 20, Armando Broja. (Guardian)
Arsenal imewasilisha ombi la pauni 50m ili kumsajili mshambuliaji wa Serbia Dusan Vlahovic, 21, huku ikimuuza kiungo wa kati wa Uruguay Lucas Torreira ili kupunguza gharama ya mchezaji huyo. (Metro)
Arsenal bado ina hamu ya kumsajili beki wa kulia wa Nottingham Forest aliyepo kwa mkopo Djed Spence lakini mchezaji huyo wa Middlesborough , 21, pia anavutia hamu kutoka kwa mabingwa wa Itali Roma na Inter Milan.. (Mirror)
Beki wa kati wa Barcelona na Uruguay anaivutia Man United , Liverpool na Chelsea huku mpango wa kutia saini kandarasi mpya ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 ukikwama La Liga. (Marca)
Leicester City inajiandaa kuondoka kwa kiungo wa kati wa Ubelgiji Youri Tielemans, 24. (Mirror)
Arsenal ina hamu ya kumsajili Tielemans, ambaye amesalia na miezi 18 katika kandarasi yake kukamilika. (Sun)





No comments:
Post a Comment