Aliyekuwa mtangazaji wa BBC ateuliwa kuwa mkurugenzi wa mawasiliano ya rais Tanzania - KABATA

This is the special room for news where you need to settle with!


Breaking

Tuesday, 1 February 2022

Aliyekuwa mtangazaji wa BBC ateuliwa kuwa mkurugenzi wa mawasiliano ya rais Tanzania

 

Mtangazaji wa zamani wa BBC Zuhura Yunus
Image caption: Mtangazaji wa zamani wa BBC Zuhura Yunus

Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amemteua aliyekuwa mwandishi wa BBC Zuhura Yunus Abdalla kuwa mkurugenzi wa mawasiliano ya rais.

Kabla ya uteuzi huo bi Zuhura Yunus alikuwa Mtayarishaji wa vipindi na mtangazaji wa idhaa ya Kiswahili ya Shirika la Uingereza BBC.

Bi Zuhura anachukua nafasi yake bwana Jaffar Haniu ambaye amepangiwa kuchukua majukumu mengine kulingana na Taarifa iliotiwa Saini na kaimu mkurugenzi wa mawasiliano ya rais.

Uteuzi wake unakuja miezi kadhaa baada ya kuandika kitabu chake cha wasifu wa Biubwa Amour Zahor mwanaharakati mwanamke wa kisiasa wakati wa mapinduzi ya Zanzibar mwaka 1964.

Zuhura alianza kama mtangazaji wa redio na mzalishaji wa vipindi mwaka 2008.

Mwaka 2014 alihamia Swahili TV na akawa mwanamke wa kwanza kutangaza Dira ya Dunia TV.

Zuhura Yunus :Mtangazaji wa BBC kuondoka baada ya kuitumikia kwa takriban miaka 14

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here