Rais wa Tanzania Samia Suluhu akutana na kiongozi wa Chadema aliye uhamishoni Tundu Lissu - KABATA

This is the special room for news where you need to settle with!

Wednesday, 16 February 2022

Rais wa Tanzania Samia Suluhu akutana na kiongozi wa Chadema aliye uhamishoni Tundu Lissu

 

TV

Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amekutana na makamu mwenyekiti wa chama cha Chadema aliye uhamishoni Tundu Lissu.

Taarifa kutoka kurugenzi ya mawasiliano ya rais inasema rais Samia alifanya mazungumzo mafupi na Lissu baada ya kukubali maombi ya kiongozi huyo wakati rais akiwa ziarani jijini Brussels.

Taarifa hiyo imesema wawili hao walizungumza kuhusu ‘masuala mbali mbali yenye maslahi na ustawi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania’

Katika ujumbe wake kupitia Twitter Zitto Kabwe wa chama cha ACT Wazalendo amesema hatimaye 'hekima imetawala na mlango wa mazungumzo kufunguka'.

Ameongeza kwamba wanaamini kama chama kuwa mazungumzo ndio njia bora ya kushughulikia tofauti za kisiasa nchini Tanzania .

Alichosema awali kuhusu kukutana na rais

Mnamo mwezi Juni mwaka jana Lissu alisema kwamba alikuwa tayari kurudi Tanzania ili kufanya kazi na Rais Samia Suluhu Hassan baada ya kwenda mafichoni nchini Ubelgiji baada ya uchaguzi wa mwaka wa 2020.

Bwana Lissu ambaye alikuwa akizungumza wakati wa uzinduzi wa kitabu chake wakati huo kuhusu demokrasia Afrika Mashariki, alisema kwamba tayari alikuwa amempigia simu rais Samia na kuomba kufanya mkutano naye.

Akizungumza wakati huo mjini Nairobi, Lissu ambaye alipoteza uchaguzi wa mwaka wa 2020 kwa Hayati John Pombe Magufuli alisema kwamba lengo lake la kupata mkutano wa ana kwa ana na Rais Samia ni kuzungumzia kuhusu kupanua hali ya kidemokrasia ambayo alisema inatia wasiwasi.

Alisema kwamba kwa rais huyo mpya kufanikiwa, mabadiliko ya kikatiba , kutoa uhuru kwa sauti za wapinzani ni muhimu .

Tundu Lissu: Nataka kuonana na Rais Samia Suluhu Hassan ana kwa ana

Miaka 60 ya uhuru: Mchango wa vyama vya upinzani katika siasa za Tanzania

Je, ACT Wazalendo kinaweza kuwa chama kikuu cha upinzani Tanzania?

No comments:

Post a Comment