Tetesi za soka Ulaya Ijumaa 18.02.2022: Mbappe, Ronaldo, Messi, Rice, Martinez, Gallagher - KABATA

This is the special room for news where you need to settle with!


Breaking

Friday, 18 February 2022

Tetesi za soka Ulaya Ijumaa 18.02.2022: Mbappe, Ronaldo, Messi, Rice, Martinez, Gallagher

 

Mbappe

CHANZO CHA PICHA,EPA

Mshambuliaji wa Ufaransa Kylian Mbappe, 23, inaaminika kubadili upepo kuelekea Liverpool baada ya kutohamasika na kiwango kilichooneshwa na Real Madrid katika mchezo wa ligi ya mabingwa Ulaa dhidi ya Paris St-Germain. (Sport, via Star)

Hata hivo PSG iko tayari kumfanya Mbappe kuwa mchezaji anayelipwa fedha nyingi zaidi duniani kwa kumpa mshahara unaokaribia £1m kwa wiki kumzuia asiondoke. (Independent)

Mshambuliaji wa Manchester United, mreno Cristiano Ronaldo, 37, anaweza kujikuta akicheza pamoja na hasimu wake mshambuliaji wa Argentina Lionel Messi, 34, msimu ujao pale Paris St-Germain. (Mirror)

Cristiano Ronaldo

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,

Cristiano Ronaldo

Real Madrid inajipanga kumsajili achezee Bernabeu mlinzi wa kushoto wa Arsenal raia wa Scotland Kieran katika dirisha la usajili ya majira ya joto. (Calciomercato, via Sun)

Manchester City inakaribia kumsajili winga wa kibrazil Savio kutoka Atletico Mineiro, tayari siku ya kufanyiwa vipimo vya afya kwa kinda huyo mwenye umri wa miaka 17 imepangwa. (Fabrizio Romano)

Matumaini ya Kiungo wa West Ham na England Declan Rice, 23, ya kujiunga Chelsea yamefifishwa baada ya Thomas Tuchel kuamua kumtumia kiungo muingereza Conor Gallagher, 22, kwenye kikosi cha kwanza cha 'Blues' msimu ujao. (Standard)

Newcastle wako tayari kupeleka ofa mpya kwa ajili ya mlinzi wa Sevilla, mbrazili mwenye miaka 28, Diego Carlos. (Marca, via Sun)

Lautaro Martinez

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,

Lautaro Martinez

Arsenal na Manchester City zinafikiria kumsajili mshambuliaji muargentina wa Inter Milan Lautaro Martinez, 24 katika dirisha lijalo la usajili. (Sun)

Bosi wa zamani wa Red Bull Salzburg na RB Leipzig, mmarekani Jesse Marsch ni chaguo la kwanza la Leeds United kuchukua nafasi ya kocha Marcelo Bielsa, 66, kama klabu hiyo itaamua kuachana na kocha huyo muargentina, mwishoni mwa msimu. (Telegraph)

Wasaka vipaji wa Newcastle United wanamfuatilia kwa karibu kinda la kimataifa la Ubelgiji Jeremy Doku, 19 ambae anachezea Rennes akitajwa kuwa na thamani ya £22m. (Chronicle)

Baada ya majaribio kadhaa ya kumsajili mlinzi raia wa uholanzi, Sven Botman, 22 kutoka Lille katika dirisha la usajili la mwezi Januari kushindwa, Newcastle United imeanza tayari mazungumzo ili kupata huduma yake katika dirisha lijalo la usajili. (Mirror)

.

CHANZO CHA PICHA,BBCSPORT

Maelezo ya picha,

Rudiger

Kwa sasa hakuna mazungumzo yanayoendelea kati ya Chelsea na wawakilishi wa mlinzi Antonio Rudiger, 28 kuhusu mkataba mpya wa mlinzi huyo wa Ujerumani ili aendelee kusalia Stamford Bridge. (Sky Sports)

Mkurugenzi wa michezo wa Sevilla Monchi anaamini kwamba Anthony Martial anafuraha nchini Hispania kufuatia mshambuliaji huyo mfaransa kuhamia timu hiyo akitokea Manchester United mwezi uliopita. (Metro)

AC Milan imeungana na Borussia Dortmund na Barcelona katika mbio za kumsajili mlinzi wa kulia wa Morocco Noussair Mazraoui, 24, ambaye alisema ataondoka Ajax mkataba wake utakapomalizika mwishoni mwa msimu. (Fabrizio Romano)

Mtendaji mkuu wa Arsenal Vinai Venkatesham ametetea uamuzi wa klabu hiyo wa kutotumia fedha kusajili katika dirisha la mwezi Januari. (Sun)

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here