Tetesi za soka Ulaya Jumanne 01.02.2022: Mbappe, Ramsey, Dembele, Botman, Aubameyang - KABATA

This is the special room for news where you need to settle with!

Tuesday, 1 February 2022

Tetesi za soka Ulaya Jumanne 01.02.2022: Mbappe, Ramsey, Dembele, Botman, Aubameyang

 

Mbappe

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,

Mbappe

Mshambuliaji wa Ufaransa Kylian Mbappe, 23, amekubali kujiunga na Real Madrid kwa uhamisho wa bila malipo wakati mkataba wake na Paris St-Germain utakapomalizika msimu wa joto. (Bild - in German)

Lyon ilijaribu kumsajili mshambuliaji wa Arsenal na Ufaransa Alexandre Lacazette wakati wa uhamisho wa wachezaji, klabu hiyo ya Ligue 1 sasa italazimika kufikia makubaliano na mshambuliaji wao wa zamani, 30,msimu wa joto. (L'Equipe - in French)

Kiungo wa kati wa Wales Aaron Ramsey, 31, alikuwa ametolewa kwa Brentford, West Ham, Aston Villa, Crystal Palace, Wolves na Arsenal kabla ya kujiunga na Rangers kutoka Juventus. (JOE)

Aaron Ramsey

Aston Villa walifikiria kumnunua kwa kima cha £50m mchezaji wa safu ya kati ya Brighton na Mali Yves Bissouma, 25, wakati wa uhamisho wa wachezaji. (Mail, via Birmingham Mail)

Villa pia walikataa ofa tatu za kumuuza kiungo wa kati wa Brazil Douglas Luiz mwezi Januari, ikiwa ni pamoja na siku ya Jumatatu, kwa matumaini kwamba kiungo huyo wa miaka 23-atakubali kusaini mkataba wa muda mrefu. (Athletic)

Everton ilifanikiwa kumnunua mchezaji wao wa zamani, na kiungo wa kati wa Senegal Idrissa Gueye, 32, kutoka Paris St-Germain dakika za mwisho kabla ya dirisha la uhamisho kufungwa. (Athletic - via Express)

Ousman Dembele

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Barcelona ilitathmini uwezekano wa kumwasilisha mshambuliaji wa Ufaransa Ousmane Dembele, 24, kwa Arsenal lakini kwa mkopo kama sehemu ya makubaliano ya kumleta mshambuliaji wa Gabon Pierre-Emerick Aubameyang,32, katika uwanja wa Nou Camp. (Independent)

Jesse Lingard wa Manchester United aliambiwa kuwa hawezi kuondoka katika klabu hiyo siku ya Jumatatu lakini kiungo huyo wa kati wa England wa miaka 29- alizuiliwa kuhama kwa mkopo siku ya mwisho ya uhamisho wa wachezaji. (Manchester Evening News)

United pia pia alizuia uhamisho wa mkopo kutoka kwa Watford kwa mlinda mlango wa Uingereza Dean Henderson, 24. (Manchester Evening News)

.

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Ombi la Chelsea la kutaka kumnunua mshambuliaji wa Charlton wa miaka 18- Mason Burstow katika dirisha la uhamisho lilikataliwa mara mbili. (Talksport - via Sun)

Mkufunzi wa Real Madrid Carlo Ancelotti ameambiwa lazima afanye upya mtihani wa Uefa wa ukocha baada ya muda wa cheti chake kukumalizika. (Corriere dello Sport - via Talksport)

Newcastle walijaribu kumsajili mlinzi wa Brazil wa miaka 32- Felipe kutoka Atletico Madrid siku ya mwisho ya uhamisho wa wachezaji. (Cadena Cope - in Spanish)

Kocha mpya Frank Lampard atakua na matokeo mazuri katika klabu ya Everton, anasema mshambuliaji wa zamani wa Ligi ya Primia Gabriel Agbonlahor. (Talksport)

Donny van de Beek, 24, aliyejiunga na Everton kwa mkopo anaamini anaweza kujifunza mengi kutoka kwa Lampard na kuongeza kuwa uteuzi wa kocha huyo wa zamani wa Chelsea ulikua muhimu katika kufikia uamuzi wake wa kuhamia Goodison Park kutoka Manchester United. (Evening Standard)

Beki wa Leicester City James Justin,23, amefaulu katika mazungumzo na klabu hiyo kuhusu mkataba mpya. (Leicester Mercury)

justin

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Mshambuliaji wa zamani wa West Ham Dean Ashton amehoji mpango wa siku zijazo za klabu hiyo baada ya kukosa kununua wachezaji waliodhamiria katika dirisha la uhamisho wa Januari. (Talksport)

No comments:

Post a Comment