Tetesi za soka Ulaya Jumanne 01/03/2022: - KABATA

This is the special room for news where you need to settle with!

Monday, 28 February 2022

Tetesi za soka Ulaya Jumanne 01/03/2022:


Victor Osimhen

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,

Victor Osimhen

Manchester United inajiandaa kulipa kitita cha £100m kumsajili mshambuliaji Mnigeria Victor Osimhen, 23 kutoka Napoli. (Star)

Manchester United imeonyesha pia nia ya kumtaka kiungo mreno wa Sporting Lisbon Joao Palhinha, ikiwatuma mara nane msimu huu tu wataalamu wake wa vipaji kumuangalia. (Record, via Sun)

Klabu ya David Beckham inayoshiriki ligi kuu ya Marekani ya MLS, Inter Miami itafanya kila linalowezekana kumsajili Lionel Messi, 34 iwapo mchezaji huyo wa kimataifa wa Argentina ataamua kuondoka Paris St-Germain mapema msimu huu. (Miami Herald, via Mail)

Messi

CHANZO CHA PICHA,REUTERS

Real Madrid inatarajia kwanza kukamilisha mpango wa kumsajili mshambuliaji mfaransa Kylian Mbappe, 23, kutoka PSG kabla ya kuanza usajili wachezaji wengine au kuwaongezea mikataba wachezaji waliopo. (Goal)

Nyota anayesakwa na Arsenal Jonathan David, 22 ana mpango wa kuondoka Lille msimu huu, ikiwapa chagizo zuri "the Gunners" kukamilisha mpango wa kumsajili mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Canada mwishoni mwa msimu. (Sky Germany, via Express)

Winga wa England Bukayo Saka ana furaha Arsenal licha ya ripoti kusema kuwa nyota huyo mwenye umri wa miaka 20 amesimamisha kwa sasa mazungumzo ya mkataba wake mpya. (Fabrizio Romano)

Bukayo Saka

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Nottingham Forest imeanza mazungumzo na kiungo Muingereza Ryan Yates, 24, ikipambana pia kumbakiza kiungo anayesakwa sana raia wa Wales, Brennan Johnson, 20 ambaye anahusishwa na Tottenham. (Mirror)

LA Galaxy wanavutiwa kumsajili mlinzi wa kati mkongwe wa hispania Sergio Ramos, 35, ambaye anahaha kuonyesha cheche na kutoa mchango mkubwa Paris St-Germain kwa sababu ya majeruhi yanayomuandama. (Foot Mercato - in French)

Ajax inataka kumteua mshauri wa michezo wa Barcelona Jordi Cruyff kuwa mkuregenzi wao mpya wa soka baada ya kuondoka kwa Marc Overmars. (Marca - in Spanish)

Zaniolo kulia

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,

Zaniolo kulia

Juventus inaongoza mbio za kumuania winga wa Italia Nicolo Zaniolo, 22 ambaye hajasaini bado mkataba mpya na klabu yake ya Roma. (Luca Bianchin via SB Nation)

Juventus pia wana matumaini ya kumbakiza mshambuliaji mhispania Alvaro Morata, 29, klabuni hapo atakapomaliza mkataba wake wa mkopo akitokea Atletico Madrid. (Gazzetta dello Sport - in Italian)

No comments:

Post a Comment