Mlinzi wa Chelsea Antonio Rudiger, 28, anasema klabu hiyo itaamua kama abakie ama aondoke mkataba wake utakapomalizika mwishoni mwa msimu. Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ujerumani ameshapokea ofa za kujiunga na Real Madrid na Paris St-Germain. (Athletic - subscription)
Newcastle itarudi na ofa mpya Sevilla katika majira ya joto kwa ajili ya kumnasa mlinzi wa Kibrazil Diego Carlos, 28, ambaye walimkosa katika dirisha la usajili la mwezi Januari. (Marca - in Spanish)
Paris St-Germain inaanda kitita kinene kwa ajili ya kumnasa kiungo mfaransa Paul Pogba katika uhamisho wa bure msimu ujao. Hata hivyo, nyota huyo mwenye umri wa miaka 28, hajakataa uwezekano wa kusalia Manchester United, huku Juventus, Barcelona na Real Madrid zikifuatilia sakata lake. (Mail)
Manchester United imemuweka Christopher Nkunku, 24, katika orodha ya wachezaji waliopewa kipaombele kusajiliwa kwenye dirisha la kiangazi baada ya kocha wa muda Ralf Rangnick kuitaka klabu hiyo kumsajili kiungo huyo mfaransa wa klabu ya RB Leipzig. (ESPN)
Cristiano Ronaldo na baadhi ya wachezaji wa Manchester hawaamini kama Ralf Rangnick ana uwezo wa kuiongoza klabu hiyo ya Old Trafford. (AS - in Spanish)
Ushawishi binafsi wa Rangnick uliingilia kati kumfanya Edinson Cavani, 35, kubadili mawazo yake ya kutimka Manchester United mwezi Januari. Hata hivyo mshambuliaji huyo wa Uruguay ataondoka mwishoni mwa msimu mkataba wake utakapomalizika. (Fabrizio Romano)
Manchester City ni miongoni mwa vilabu vya ligi kuu England vinavyomfuatilia kiungo wa Barcelona na timu ya taifa ya Hispania ya U-21 Nico Gonzalez, 20, ambaye amekua akifanya vizuri Nou Camp msimu huu. (Marca - in Spanish)
Arsenal ilikataa fursa ya kumsajili mshambuliaji wa Argentina Mauro Icardi, 28, kutoka Paris St-Germain wakati wa dirisha la usajili la mwezi Januari. (Athletic - subscription)
Mshambuliaji wa Chelsea na Albania Armando Broja, 20, hapuuzi uwezekano wa kutimka Stamford Bridge msimu huu huku Arsenal ikitaka kumsajili kutokana na kiwango bora alichoonyesha pale Southampton anakocheza kwa mkopo. (The Express).
Klabu ya Serie B Como na baadhi ya timu kutoka ligi kuu Uturuki zimeonyesha nia ya kumsajili Jack Wilshere, 30, ambaye amekua akifanya mazoezi na klabu yake ya zamani ya Arsenal na mara ya mwisho kuichezea England ilikuwa mwaka 2016. (Football London)
Kiungo wa Ivory Coast Franck Kessie, 25, hajaamua klabu gani atajiunga nayo baada ya mkataba wake na AC Milan kumalizila mwishoni mwa msimu huku Barcelona ikionyesha pia nia ya kumsajili. (Fabrizio Romano)
Kiungo wa zamani wa Manchester United Paul Ince anasema klabu hiyo inapaswa kumsajili kiungo wa Brighton na Mali Yves Bissouma, 25, kuchukua nafasi ya kiungo wa kimataifa wa Brazil Fred, 28, kwenye eneo muhimu la kati. (Metro)





No comments:
Post a Comment