Tetesi za Soka Ulaya Jumanne 22.02.2022:Pochettino, Silva, Bowen, Rodgers, Kilman, Mbappe - KABATA

This is the special room for news where you need to settle with!


Breaking

Monday, 21 February 2022

Tetesi za Soka Ulaya Jumanne 22.02.2022:Pochettino, Silva, Bowen, Rodgers, Kilman, Mbappe

 

Mauricio Pochettino

Real Madrid watachuana na Manchester United katika kumnasa kocha wa Paris St-Germain Mauricio Pochettino. (Mail)

Kiungo wa kati wa Manchester City na Ureno Bernardo Silva, 27, ana ndoto ya kuhamia Real Madrid. (CalcioMercato in Italian)

Bernardo Silva

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Kocha wa Leicester Brendan Rodgers anaungwa mkono na bodi ya klabu hiyo licha ya mwenendo mbaya. (Telegraph)

Liverpool "wana nia ya dhati" kumsajili mshambuliaji wa Uingereza Jarrod Bowen, 25, kutoka West Ham. (NipeSport)

Jarrod Bowen

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Inter Milan wanamfuatilia mshambuliaji wa Manchester City na Brazil Gabriel Jesus, 24, usajili muhimu kwa safu yao ya ushambuliaji. (CalcioMercato - in Italian)

Chelsea wanavutiwa na mlinzi wa Wolves, Muingereza Max Kilman, 24. (Talksport)

Max Kilman

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Arsenal, Newcastle, Borussia Dortmund na Inter Milan wanatazamia kumnunua mshambuliaji wa Lille na Canada Jonathan David, 22. (TuttoMercatoWeb - in Italian).

Aston Villa wamemfanya mlinzi wa Liverpool na England Joe Gomez mwenye umri wa miaka 24 kuwa lengo lao kuu msimu wa joto. (Football Insider)

Liverpool wako nje ya mbio za kumnunua mshambuliaji wa Ufaransa Kylian Mbappe, 23, kutoka Paris St-Germain. (Sport)

Kylian Mbappe

CHANZO CHA PICHA,EPA

Tottenham itasubiri kuanza mazungumzo na mshambuliaji wa Uingereza Harry Kane, 28, kuhusu kandarasi mpya. (Athletic - subscription required)

Mlinda mlango wa Manchester United na Uhispania David De Gea, 31, anasema yuko tayari kusaini mkataba mpya na klabu hiyo. (Independent)

David De Gea

CHANZO CHA PICHA,REUTERS

Kiungo wa kati wa Uingereza Jonjo Shelvey, 29, na mlinzi wa Uswizi Fabian Schar, 30, wako mbioni kusaini kandarasi mpya huko Newcastle. (Telegraph)

Roy Keane, 50, alikataa nafasi ya kuwa kocha wa timu ya League One ya Sunderland kwa sababu walimpa tu kandarasi ya miezi sita na alitaka zaidi. (Sun)

Roma haitampa kiungo wa kati Muingereza Ainsley Maitland-Niles anayecheza kwa mkopo kutoka Arsenal mkataba wa kudumu kwa sababu hajafanya vizuri kwenye Serie A. (Calciomercato, via Mirror).

Ainsley Maitland-Niles

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Wembley inaweza kuandaa fainali ya Ligi ya Mabingwa msimu huu ikiwa Uefa itaamua kuiondoa St Petersburg kwa sababu ya mzozo wa Urusi na Ukraine. (Mirror)

Matumaini ya Newcastle, Leeds na Crystal Palace kumsaini kiungo wa kati wa Wales Brennan Johnson, 20, yamefifia huku Nottingham Forest wakiongeza juhudi zao za kumpata kusaini mkataba mpya. (Mirror)

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here