Tetesi za soka Ulaya Jumatano 02.02.2022: Haaland, Rice, Ruiz, Botman, Carvalho, Dembele, Gil - KABATA

This is the special room for news where you need to settle with!

Tuesday, 1 February 2022

Tetesi za soka Ulaya Jumatano 02.02.2022: Haaland, Rice, Ruiz, Botman, Carvalho, Dembele, Gil

 

Erling Braut Halaanda

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Manchester City "itafanya kila iwezalo kumshawishi mshambuliaji wa Borussia Dortmund Erling Braut Haaland kujiunga na klabu hiyo mwisho wa msimu huu , licha ya kwamba mshambuliaji huyo wa Norway angefaa kuhamia klabu ya Real Madrid. (Athletic, subscription required)

Haaland, 21, hatahivyo anadaiwa kwamba hayuko katika mipango ya Real Kwasasa , huku klabu hiyo ya Uhispania badala yake ikitaka kumsaini mshambuliaji wa PSG Kylian Mbape , 23 mwisho wa msimu huu (El Chiringuito, via AS in Spanish)

Mshambuliaji wa Serbia Serbia Dusan Vlahovic, 22, anasema kwamba ilikuwa uamuzi rahisi kuipuuza Arsenal na kujiunga na Juventus wakati wa dirisha la uhamisho la mwezi Januari. (Metro)

Dusan Vlahovic

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Kiungo wa kati wa West Ham, 23 na England Declan Rice, 23, beki wa kati wa Sevilla Jules Kounde na mchezaji mwenzake Aurelien Tchouameni, 22, kutoka Monaco, wameorodheshwa na mkufunzi wa Chelsea kama wachezaji wanaolengwa na timu hiyo mwisho wa msimu huu (Athletic, subscription required)

Ombi la Newcastle United la dau la £40m kumsajili kiungo wa kati wa Napoli na Uhispania ,25, Fabian Ruiz limekataliwa , lakini The Magpies wanatarajiwa kuimarisha lengo lao mwisho wa msimu huu. Arsenal inasemekana kuonesha hamu ya kumsajili mchezaji huyo.(Corriere dello Sport - in Italian)

Mkufunzi wa Newcastle Eddie Howe pia atawasilisha ombi la kumsajili Sven Botman, 22, mwisho wa msimu baada ya kumkosa beki huyo wa Lille na Uholanzi kwa dau la £35m. (Mirror)

Carvalho

Liverpool ina matumaini ya kukamilisha usajili wa mapema wa mshambuliaji wa Fulahm Fabio Carvalho 19, kama mchezaji huru mwisho wa msimu huu baada ya kumkosa mchezaji huyo wa Portugal katika siku ya miwsho ya dirisha la uhamisho.. (Sky Sports)

West Ham ilishindwa katika siku ya mwisho ya dirisha la uhamisho kumsaini mshambuliaji wa Colombia Duvan Zapata, 30, kwa mkopo kutoka klabu ya Itali Atalanta. (Sky Sports)

Rais wa klabu ya Barcelona Joan Laporta anaamini winga wa Ufaransa Ousmane Dembele, 24, amekubali kuafikia mkataba na klabu nyengine kama mchezaji huru mwisho wa msimu huu wakati kandarasi yake katika klabu ya Barcelona itakapokamilika. (Goal)

Ousmane Dembele

Barca inafikiria kuifuta kandarasi wa Dembele mapema hatua ambayo huenda ukaifanya klabu ya Chelsea , Tottenham na PSG kuimarisha hamu yao kumsajili winga. (Express)

Winga wa Uhispania Bryan Gil, 20, alisema kwamba familia yake ilimtaka kurudi Uhispania kuichezea klabu ya Valencia kwa mkopo miezi sita tu baada ya kujiunga na Tottenham kutoka Sevilla kwa £21m. (Sun)

Aliyekuwa mkufunzi wa zamani wa Ujerumani Joachim Low amekubali kuchukua ukufunzi wa klabu ya Uturuki Fenerbahce, huku kocha huyo aliyeshinda kombe la dunia ,61 akitarajiwa kuchukuwa uongozi wa klabu hiyo kabla ya kuanza kwa msimu ujao.. (Haber Global, in Turkish)

.

CHANZO CHA PICHA,PA MEDIA

Beki wa Newcastle Jamal Lewis, 24, anadaiwa kukataa ombi la kuhamia katika klabu ya Stoke na Birmingham City, na sasa huenda akawachwa nje katika kikosi cha wachezaji 25 cha klabu hiyo ili kutoa nafasi kwa wachezaji watakaosajiliwa mwezi Januari. (Football Insider)

No comments:

Post a Comment